![]() |
| Bwana Huruma Kissaka. |
![]() |
| Kutoka kushoto ni Bwana Kissaka, diwani kata Miembeni Bwana Richard Gasper, mwenyekiti wa mtaa Peps na Bi Innosensia afisa Ugani wa kata. |
![]() |
| Wajumbe wakimsikiliza mwenyekiti akitoa utambulisho. |
![]() |
| Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mtaalamu |
![]() |
| Ni sehemu ya baraba wanayotarajia kujenga kwa kiwango cha lami kata miembeni |
Bank ya dunia inatarajia
kujenga barabara za lami katika manispaa ya Bukoba, ambapo mpembuzi yakinifu
kutoka kampuni yaHaworld Hamphrey Ltd ya jiji Dar es salaam Bwana Huruma
Kissaka, amefanya mazungumzo ya awali na wananchi ili kujua kamawanaunga mkono ujenxi
wa barabara ya kata Miembeni kuanzia TX hadi Mafumbo kupitia Nyamkazi.
Katika.mazungumxo hayo,
mthamini huyo alitaka kujua kama maeneo lengwa yanauwezekeano wa kupata mita 9
hadi 10 katika barabara iliyopo ili kuondoa malalamiko ya wananchi kujitokeza
baada ya kuanza ujenzi huo kwani barabara itakuwa ya kiwango cha juu na
wananchi wanaweza kulalamikia vifaa vya kushindilia kuwa vimebomoa nyumba zao.
Katika mkutano huo kwa wakazi
wa Miembeni mtaa wa Peps, wakazi wamesema kuwa barabara wanaitaka isipokuwa
wameshauri kuwa barabara iliyopo sasa imekaa pembeni kweneye makazi ya watu,
hovyo wakianza ukarabati wa Bnk ya dunia wahamishie katika maeneo husika
yaliyopimwa na serikali ili kuondoa malalamiko ya baadhi ya wananchi
kuhijltajifidia.
Bank ya dunia. inatarajia
lujenga barabara yenye jumla.ya urefu wa kilomita 12 katika manispaa ya Bukoba
ikiwemo Kashai, Chemba hadi Kibeta na maeneo mengine katika manispaa hiyo, ila
akiwataadhalisha wananchi kuwa banki ya dunia haiitaji malalamiko ya wananchi
kidai fidia kwani wao hawatoi fidia.
Na Mwanaharakati.






No comments:
Post a Comment