MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 24 April 2014

BARABARA ILIYOGHARIMU ZAIDI YA MILIONI 100, YAANZA KUHARIBIKA KABLA YA KUKABIDHIWA BUKOBA

 Ni ile inayoanzia Gereza Rwamulumba kata Karabaigaine hadi Kanazi kata Bujugo Bukoba vijijini, ambapo wananchi walifuraia ujenzi wa barabara hiyo kwani imekua historia tangu wamekuwapo hawajawahi kuwa na barabara badala yake kulikuwa na njia yenye makorongo, na kusababisha vifo vya wagonjwa na akina mama wajawazito kutokana na kushindwa kupitisha gari, ilhali vituo vya afya vikiwa mbali nao.
Hata hivyo barabara hiyo iliyomalizika kujengwa mwishoni mwa mwaka jana, inaharibika kutokana na wakandarasi kuweka CALVAT pasipokujua historia yake ambapo wameweka sehemu hisiyo na matatizo na kuacha yanapohitajika kama picha zinzvyoonesha.

Akizungumza na mtandao huu, mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba Bwana DAUDA KATEME, amesema kuwa kwakuwa wamepata taarifa watahakikisha wanakabidhiwa kazi iliyokamilika na ya viwango, japo awali kabla ya kukamilika kwake, aliueleza mtandao huu kuwa wataikabidhi mwezi wa 12 mwaka jana.

Na Mwanaharakati.

No comments: