![]() |
| Bouteflika |
Taarifa kutoka nchini Algeria
zinasema kuwa Rais Abdelaziz Bouteflika ameshinda uchaguzi mkuu uliofanyika
mnamo siku ya Alhamisi.
Hata kabla ya matokeo kutangazwa, kiongozi wa chama rasmi cha upinzani Ali Benflis, alisema kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi.
Bouteflika, ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 15, anakumbwa na hali mbaya ya kiafya kwani anaugua kiharusi na alipiga kura akiwa katika kiti cha magurudumu.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment