KITUO cha kurusha matangazo ya radio cha dini ya Kiislamu
cha Alnoor Zanzibar kimeteketea kwa moto ikiwemo studio zake tatu. Mkurugenzi
mkuu wa Radio Alnoor, Mohamed Suleiman Tall, alithibitisha kutokea kwa ajali
hiyo ambayo alisema chanzo chake kikubwa ni hitilafu ya moto katika kituo kikuu
cha umeme.
Alisema moto huo ulianzia katika studio nambari tatu ambayo
imeteketea huku vifaa vyote ikiwemo kompyuta pamoja na vifaa vingine muhimu vya
mawasiliano ya redio vimeteketea.
"Radio Alnoor imeteketea kwa moto ambapo studio zake
tatu zimeharibika na tunakisia tumepata hasara Sh milion 82," alisema,
juhudi za kiufundi za kurudisha matangazo ya Radio Alnoor hewani kwa
wasikilizaji wake zinaendelea hadi sasa.
"Tunafanya kila juhudi kuona kwamba wananchi wanapata
matangazo ya Radio Alnoor, licha ya kujitokeza kwa hitilafu kubwa ya studio
zake kuteketea kwa moto," alisema.
Kwa mujibu wa maelezo ya mtangazaji mmoja Rashid Salum,
alisema tukio hilo limetokea majira ya saa nane za usiku huku chanzo kikubwa ni
hitilafu za umeme.
Mmoja ya watangazaji wake Abubakar Fakih, amejeruhiwa kwa
kuumia mguu baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili kwa ajili ya kujihami na
moto huo.
"Moto ulikuwa mkubwa kiasi nililazimika kujirusha
kutoka ghorofa ya pili hadi chini kwa ajili ya kujiokoa," alisema Fakih.
Radio Noor ni maarufu visiwani hapo ambayo hurusha matangazo
yake zaidi yenye muelekeo na kutoa Elimu ya dini ya Kiislamu
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment