Ni mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), John Heche,alipovamiwa nyumbani kwake Mabibo Loyola, jijini
Dar es Salaam, imevamiwa na watu wasiojulikana, ambapo vitu vyenye thamani ya
zaidi ya sh milioni 10 vimeibwa.
Tukio hilo limetokea wiki iliyopita muda mfupi baada
ya Heche kutoka nyumbani kwake alfajiri kwenda katika kituo cha mabasi ya
mikoani cha Ubungo, kuwahi usafiri wa kwenda jijini Mwanza.
Tayari tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi
Mabibo Mwisho na kupewa kumbukumbu namba MAB/RB/225/2014, kabla ya
kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi Urafiki na kupewa namba
URP/RB/2785/2014.
Hata hivyo tukio hilo limeanza kuhusishwa na masuala ya
kisiasa hususan katika vitu vinavyodaiwa kuibwa na namna Jeshi la Polisi Kituo
cha Urafiki wanavyolishughulikia.
Vitu vilivyoibwa ni pamoja na Friji, radio, TV, Decoder ya
Dstv, jezi za mpira jozi 32, mipira 56, magodoro, meza ya TV na music system
inayotumika kwenye mikutano ya hadhara.
Hadi sasa tayari mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kuhusika
na tukio hilo amekamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo pamoja na wenzake
ambao bado wanaendelea kusakwa.
“Yule aliyekamatwa amekiri mbele ya Polisi kuhusika na tukio
na akawataja wengine sasa tunashangaa kigugumizi cha Polisi katika hili ni nini
mpaka wanashindwa kuwafuatilia na kubaini sababu zilizowafanya waibe hapa,”
alisema mmoja wa majirani wa Heche.
Heche ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
alipoulizwa iwapo anaweza kulihusisha tukio hilo na shughuli zake za kisiasa,
alisema ni mapema kuhusisha tukio hilo na siasa moja kwa moja.
“Silihusishi moja kwa moja na siasa lakini namna askari wa
Kituo cha Polisi Urafiki wanavyolichukulia kiwepesi ndiyo inanipa shaka,”
alisema Heche
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Camilius Wambura,
alipoulizwa kama analijua tukio hilo alisema hana taarifa nalo na kwamba
atafuatilia kujua kama lipo.
>>>>>Tanzania daima
>>>>>Tanzania daima
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment