Watu kumi 10 wamenusurika
kifo baada ya boati ya mizigo MV matata iliyokuwa imesheeni tani 280 za sukari
ikitoka mkoani kagera kuelekea mkoani mwanza kuzama katikati ya ziwa Victoria.
Kuzama kwa boti hiyo yenye
nambari za usajili MV 1105 mali ya
KITANO CHACHA BUNANKA kumefuatia hali mbaya ya hewa katika ziwa Victoria.
Akizungumzia tukio hilo
bwana KITANO ambaye ni mmiliki wa boti hiyo amesema watu hao 10 wamenusurika
kwa kutumia boti za dharula zilizokuwemo ndani ya boti hiyo.
Kwa mujibu wa Kitano Boti
hiyo MV matata ilianza kufanya zake katika ziwa Victoria toka mwaka 2010 ambapo
mpaka inazama imehudumu kwa muda wa miaka mitatu tu katika ziwa hilo.
Kamanda wa polisi mkoa
kagera GORGE MAYUNGA alipo hojiwa juu ya tukio hilo amesema kuwa amesikia tukio
hilo lakini hana taarifa rasmi na kusema kuwa uenda limetokea katika ziwa
Victoria upande wa mkoa wa Mwanza.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment