Ni usiku wa kuamkia leo ambapo taarifa inasema kuwa wananchi hao watatu wameuawa baada ya mapigano ya vijiji viwili tofauti katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Kamanda wa polisi mkoani humo, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo huku akisisitiza kuwa vimetokana na mapiganao kuhusu wizi wa mifugo ya ng'ombe na hiyo amesema ni kujichukulia sheria mikononi jambo ambalo ni kosa hivyo uchunguzi zaidi unaendelea na watakaobainika kuhusika hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Niko katika kufuatilia zaidi taarifa hii undani utakuja hapahapa
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment