MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 13 April 2014

WALIOFARIKI DAR KWA MAFURIKO WAONGEZEKA HUKU DARAJA KUUNGANISHA DAR- BAGAMOYO LAJENGWA

Kushoto picha ikionesha mafuriko Dar es salaam, kulia Scaveter katika ukarabati daraja Goba
Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.

Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema  watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.

Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.
Hali ya daraja wakati limebomoka
Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wameshindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.

Wakati jitihada zikifanyika kurudisha mawasiliano ya barabara na makamanda wakitafakari juu ya kuweka daraja la muda, watu wameanza lawama eti mkandarasi. Lakini ukweli ni mambo ni matatizo yetu wenyewe.
 Na Mwanaharakati.

No comments: