MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 10 May 2014

BREAKING NEWS!!!KUFUKUZWA KWA ASKARI POLISI 212 WA MAFUNZO KISA HIKI HAPA

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,mkuu wa taaluma na utumishi wa jeshi la polisi cp THOBIAS ANDENGENYE, amesema kuwa wamebainika wakitumia vyeti vya kugushi. Alisema walishirikiana na baraza la mitihani la taifa NECTA kufanya uhakiki ambapo amesisitiza kuwa uchunguzi utaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe, pamoja na kuwa wamefukuzwa kwenye mafunzo.

Kutokana na tabia hiyo, amesema kuwa wataendelea kufanya uchunguzi hata kwa wengine ili kujua kama wapo ambao tayari wameshajipenyeza lakini pia kuwaomba wenye taarifa za wengine kushirikiana na jeshi la polisi.

Kikosi cha wanafunzi wa jeshi hilo kilikuwa 3415 walioanza mafunzo tangu Desemba mwaka jana.
Na Mwanaharakati.

No comments: