MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 29 June 2014

MISS GEITA 2014; AIBUKA RECHAL KWILA




SHINDANO la kumpata mrembo wa mkoa wa Geita, Miss  Redds Geita 2014 limefikia tamati kwa Recho Kwila kuibuka mshindi wa Taji hilo.

Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi Disire  mkoani humo kwa kuwashilikisha walimbwende 11 kutoka wilaya za mkoa wa Geita, lengo kubwa likiwa niku mpata mlibwende wa kuuwakilisha mkoa wa Geita.

Akizungumza katika Tamasha hilo, mgeni rasimi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Geita Omari Manzie Magochie, aliwataka wazazi na walezi kuwaachia watoto wao kujiunga ulimbwende kwani si huuni kama wanavyo fikilia na kusema  ni kazi kama kazi Nyingine.

Naye mshindi huyo akizungumza baada ya kupata taji hilo, alisema kuwa yeye atajitaidi kuwasaidia watoto wanao wa mitaani, na kutangaza Vivutio  vilivyopo katika mkoa wa Geita kikiwemo kisiwa cha Rubondo  na Madini,  ili wageni  wanaokuja wajue kilichopo katika mkoa huo.

 Na Mwanaharakati.

ASKOFU AFUKUZWA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUWADHALILISHA WATOTO.

 

BALOZI wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya Kanisa Katoliki kwa tuhuma za kudhalilisha watoto.

Kutokana na kutiwa hatiani huko amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa na Papa kutiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ya kupokwa upadri.

Taarifa ya Vatican ilisema Monsinyori Wesolowski alikutwa na hatia na Mahakama hiyo ya Usharika wa Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa adhabu hiyo ina maana hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.

Wesolowski amepewa miezi miwili ya kukata rufaa. Lakini pia anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa nchi hiyo.

Papa alimrejesha Vatican, Wesolowski ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21, 2013 na kumfuta kazi baada ya Askofu wa Santo Domingo, Kadinali Nicolas de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri ya Dominica.

Mamlaka za Dominican hatimaye zilianza uchunguzi lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya Wesolowski.

Wesolowski ni Ofisa wa Juu Vatican kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto na kesi yake iliibua waswali iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na kuanzisha uchunguzi wake kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.

Hata hivyo Vatican haijawahi kusema iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi kutoa mawasiliano yoyote kwa mawakili wake.

Kesi hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa umakini kwani Wesolowski alipewa upadirisho wake na Uaskofu na Papa St John Paul 11 ambaye pia ni Raia wa Poland.
Na Mwanaharakati.

Friday, 27 June 2014

DIAMOND PLATNUMZ, AKANA NA KUFAFANUA WIZI WA NYIMBO ZA WASANII WENZAKE


Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno  ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea yake.



Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambao anasema baada ya kuimba wasanii wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake. 
 
Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo.
 
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo.
 
“Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
Na Mwanaharakati.

BAJETI YA UMOJA WA AFRIKA: RAIS KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI ZA UMOJA WA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika Mjini Malabo, Equatorial Guinea. Miongoni mwa masuala muhimu yanayotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huu ni bajeti ya umoja huo na mkakati wa kukusanya maoni kutoka nchi wanachama kuhusu Afrika ifikapo mwaka 2063, ambapo umajo huu utafikisha miaka mia moja.
Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wakiwa kwenye picha ya Pamoja.(Picha na IKULU).
 Na Mwanaharakati.