Taarifa zilizotufikia hivi punde, zinasema kuwa polisi wilayani Muleba wametumia mabomu hayo ya machozi baada ya wananchi kuvunja mochwari ya hospitali ya wilaya hiyo, kwa lengo la kuchukua maiti yao.
Hatahivyo polisi wamemjeruhi mwandishi wa habari na mwakilishi wa Mwananchi Communication Shaaban Ndyamkama wakati akipiga picha za tukio hilo.
Inasemekana watu kadhaa wamekamatwa kuhusu vurugu hizo baada ya wananchi kujiunda kukabiliana na polisi hao walioanza kufyatua mabomu ya machozi wakati wa tukio hilo.
Tutakuletea undani, endelea kufuatilia hapa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment