|
Mwandishi Mac Ngaiza akisoma maelezo kwenye ubao. |
Hii ni kauli mbiu iliyochorwa kwenye mabango ya barabara kuelekea Kata Bisheke, ikiamasisha jamii kupanda mbegu elekezi.
|
Mfano wa shamba la muhogo |
|
Muhogo uliokwisha pitia hatua ya kukatwakatwa baada ya kuvunwa na kumenywa. |
|
Baadhi ya wanakikosi kazi nyuma yao ni muhogo ulioanikwa baada ya hatua za kwanza |
|
Mmmoja wa wanakikundi kushoto akihojiwa na Mac Ngaiza. |
|
Mwanamama akipanga mafungu ya nyanya, kila moja sh 200 |
|
Mwenyekiti wa kikundi kazi akihojiwa na mwandishi Mac |
Kutokana na magonjwa yaliyoyakumba mazao ya migomba,
na mihogo mkoani Kagera, wakaazi wanaishi kwa shida baada ya kukosa chakula cha
kutosha ilhali wakikabiliwa na ukata wa fedha, hivyo jamii zenye watu wengi
kushindwa kuzitunza kwani kiasi kikubwa cha achakula huitajika huko vijijini.
Kutokana na hali, zipo kata zenye idadi kubwa ya
watoto chini ya miaka 5 kuliko watu wazima, hivyo kumeonekana uhitaji mkubwa wa
chakula kwa uzalishaji wao ni mdogo.
Nimetembelea kata za Mubunda na Bisheke wilayani
Muleba, ambapo kata ya Mubunda ina wakazi 1700, ambapo watoto chini ya miaka
mitano ni 12000, watu wazima wenye uwezo wa kuzalisha ni 5000 tu.
Katika kata ya Bisheke wanavijiji 13 vya kata hiyo, wameanzisha mpango wa
kilimo cha mhogo, baada ya kuletewa mbegu mpya inayokomaa kwa miezi 14 na kutoa
chakula kingi amayo wamepewa mbinu ya kuisindika baada ya kuvuna ili watumie
zao lake kwa matumizi mbalimbali.
Wananchi hao wanasema kuwa wameanza kushirikiana na
katika kikundi ambacho hawajakipa jina, kuwa wanalima mashamba na kupanda mhogo
huo ambao wamevuna kwa mara ya kwanza na zao lake ni hili hapa pichani.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment