MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 17 June 2014

WAKE WA VIGOGO WAFANYISHWA NGONO NA WAGANGA WA KIENYEJI DAR

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya  waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo  hivyo  vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi  mbalimbali ikiwemo  Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema  Kamanda Kiondo.
Baadhi ya nguo za ndani zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa ngono na Sangoma hao.
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito  baada ya kukaa  muda  mrefu  bila watoto,  wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya wanawake  hao umebaini kuwa,  waume wao wanafanya kazi  katika nyadhifa za  juu serikalini, wengine ni wastaafu  na kwamba waume hao  hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa Sangoma hao.
Kamanda Kiondo akionyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
Baadhi ya waliokamatwa katika zoezi hilo akiwamo Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.

Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani  ‘kufuli’ za  wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa  na polisi  kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.


“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa  baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.

Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao  yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema  ni  kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi  10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.

Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
Na Mwanaharakati.

No comments: