SERIKALI Wilayani Ngara mkoani
Kagera imepiga marufuku uuzaji wa pombe nyakati za usiku baada ya kukithiri kwa
matukio makubwa ya kuhatarisha usalama wa wananchi yakiwemo ya watu
kubakwa na kujinyonga.
Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine
Kanyasu ametoa agizo hili leo June 2 kwa watendaji wote wa vijiji na kata
wilayani humo kufuatia matukio ya watu kujinyonga kuongezeka na kuhatarisha
mtafaruku wa kiusalama.
Kanyasu amesema kuwa zaidi ya watu
10 wilayani humo kwa mwezi mei wamefariki kwa kujinyonga huku matukio matatu ya
ubakaji yakitokea ambapo watu watatu wamefikishwa mahakamani kwa kujaribu
kujinyonga.
Amesema wanaofanya na kufanyiwa
matukio hayo wamekuwa wakitokakwenye vilabu vya pombe nyakati za usiku na
wengine wamepoteza maisha kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa maish.
Pamoja na agizo hilo amevitaka
vyombo vya ulinzi kuhakikisha vinavunja vilabu vya pombe ambavyo vitakaidi amri
ya serikali kwa kuwafungia wateja ndani huku wakiendelea na biashara ya kuuza
pombe usiku.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment