Warembo 18 kutoka Mikoa
ya Kanda ya Ziwa wanashiriki mashindano ya Taji la Miss LAKE ZONE mwaka
2014 wametembelea kituo cha watoto yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mtaa wa
Mbugani Wilayani Geita mkoani humo na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya
shilingi laki 350,000/=, na wameonekana mfano wa kuigwa kwa kufanya usafi
katika mji wa Geita.
Wakizungumza na mtandao
huu, wamesema kuwa wameamua kufanya usafi katika mji huo ikiwa ni kutekeleza
agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo Omary Mangochie, ya kuweka mji katika hali ya usafi
kwa kufanya usafi kila Alhamisi.
Mamiss hao wamemshukuru
mdhamini wao Leonard Bugomola, ambaye ametoa vyumba 10 vya kulala, kila chumba ikiwa
ni shilingi 80,000/= kwa kila siku, na chakula chenye thamani
Tsh 15,000 kwa kila mshiriki huku wakiishi hotelini kwake kwa siku kumi
wakiwa kwenye mazoezi.
Mdhamini huyo Leonad
Bugomola ambaye ni mfanya bishara mkoani humo, amesema kuwa ameamua kutoa
zawadi hizo kutokana na Mungu kumjalia alivyo navyo na kuwa na kipaji cha
kupenda michezo mbalimbali.
Bugomola aliwaomba
wafanya biashala wenzake wa mkoa wa Geita kujitolea kwa kudhamini Mamiss
na kuacha Dhana ya kuwa Umiss ni uhuuni kwani Umiss ni ajira kama ajira
zingine.
Shindano la kumpata Miss
Lake Zone, litafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu wa nane (8), mbapo mshindi
wa kwanza atajinyakulia zawadi ya Gari.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment