MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 23 August 2014

MUHIMU: TAARIFA ZA UGONJWA WA EBOLA, SHEKH MKOANI KAGERA AWATAKA MAHUJAJI KUISIKILIZA WIZARA HUSIKA.



Mahujaji  wa Dini ya Kiislamu mkoani Kagera wanaotarajiwa kwenda HIJJA, wametakiwa kufuata utaratibu utakaowekwa na Wizara ya afya baada ya kuibuka kwa ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika ya Magharibi.

Shekhe wa mkoa Kagera HARUNA KICHWABUTA,  amesema kuwa mahujaji wanatarajiwa  kwenda SAUD ARABIA katika mji wa MAKKA kwa ajili ya hija Septemba 25 mwaka huu.

Shekhe  KICHWABUTA amesema kuwa kabla mahujaji hao kuondoka watatakiwa kufuata utaratibu utakaowekwa na serikali kupitia Wizara ya Afya ili kuepukana na hadha zinazoweza kujitokeza.

Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na nchi nyingine bado wanaendelea kulifanyia kazi suala hilo baada ya kuibuka kwa ugonjwa huo na hivyo kuwataka MAHUJAJI kuendelea kujiandikisha na kulipa gharama za usafiri.

Kadhalika Shekhe KICHWABUTA  amewataka mahujaji hao kufuata maelekezo ya mtume MUHAMAD katika kutekeleza nguzo hiyo muhimu ya Uislamu.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: