Mama mmoja
ameamua kumchanja kwa Nyembe mwanae mwenye umri wa wiki mbili baada ya mtoto
huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.
Tukio hilo
limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina la Anastazia
Ngilitu kumchana mwanae kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia kupata haja
kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya haja
kubwa.
Mama
huyo mkazi wa Tabora aishie jijini Mwanza kwa sasa, amesema kuwa alijifungua
watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro
kisha wawili kufariki walipofikishwa Hospitali na kusalia mtoto mmoja
aliyekutwa na tatizo la
kukosa
sehemu ya haja kubwa.
Sambamba
na hayo, mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na mwanawe ni baada ya
kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali iliyosababisha tumbo
kujaa upande wa kulia.
Katika
hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo nzuri,
kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali alikuwa
anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa hawezi kutokana
na kuwa na mtoto mdogo.
Sambamba
na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa wakati
tofauti, na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine kumdhurumu pesa,
zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi
halijakaza, hali anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu
nyingi baada ya mumewe kumpiga.
Kitendo
cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe
kinatoakana na hofu ya kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa
kwani kwa sasa yeye mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto
na alipoenda Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi
elfu 30 na alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za
kienyeji.
Kwa
upande wao baadhi ya majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa
mara,Wameiambia wanasema kuwa ana maisha magumu kwani mume wake humpiga na
kumfukuza mara kwa mara hali inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati
mwingine kulala na watoto wake bila kula.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment