POMOJA na Serikali kuendelea kupiga marufuku kuwepo
kwa waganga wa kienyeji matapeli na wenye nia mbaya katika Nchi yetu ya
Tanzania bado suala hilo linazidi kupamba moto kwa kuibuka waganga hao
katika Mkoa wa Geita.

Wakiongea kwa Nyakati Tofauti baadhi ya wananchi wa
kata hiyo kwa shariti la kutotaka kutajwa majina yao walisema kuwa Diwani huyo
amekuwa akiwapigia Ramli chonganishi watu wanaokwenda kwake kwa ajili ya kupata
tiba ya kienyeji hivyo kuwaomba wanaohusika kuchukua hatua dhidi ya Diwani
huyo.
Wananchi hao wameongeza kuwa Diwani huyo amekuwa ni kero kwa
watu kwani amekuwa akiwatapeli watu kwa kuwapatia Tiba za uwongo na kuwa
chonganisha watu bila kuona kuwa yeye ni kiongozi.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Juma Choba alikiri
kukamatwa kwa Diwani wake lakini akasema kuwa alikamatwa kwa tuhuma
za kuwaosha wakataji wa mapanga katika kata hiyo lakini akasema kuwa
hajui kama ni kweli anafanya kazi hiyo kwani hajawahi kuona ila anasikia kutoka
kwa wananchi kuwa diwani wake anawapigia ramli chonganishi.
Mimi nasikia kama wewe unavyosikia lakini sijawai kumuona
ila amekamatwa yuko Polisi Wilayani inawezekana ni kweli kwa kweli siwezi
kukataa alisema Mtendaji huyo.
Alipoulizwa Diwani Mawazo kuhusu kukamatwa kwake na kupiga
ramli chonganishi alisema kuwa yeye ana lolote la kujibu juu ya hilo.
Jeshi la polisi Mkoani hapa limethibitisha kukamatwa
kwa Diwani Mawazo na uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hilo .
Na Mwanaharakati./Na. Valence Robert Geita.
No comments:
Post a Comment