MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 17 September 2014

MWANAHABARI ACHAGULIWA KATIKA SAFU YA UKATIBU CHADEMA

 


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amewateua Dk. Willbrod Slaa kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalim ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
 
Viongozi hao wameteuliwa jana usiku na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema hivyo kufikia tamati ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.
 
Mhe. John Mnyika anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama hicho kwa kudaiwa kuvunja katiba ya chama.

Na Mwanaharakati.

No comments: