KAULI ya Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe ya kuagiza yafanyike maandamano na migomo nchi nzima bila kikomo,
ikiwezekana hata bila ya kibali cha Polisi, imelichefua Jeshi la Polisi.
Jeshi hilo limeonya kuwa halitasita kumchukulia hatua kali, kwa kuwa anavuka mipaka ya kisiasa na kugeukia makosa ya jinai.
Jeshi hilo limeonya kuwa halitasita kumchukulia hatua kali, kwa kuwa anavuka mipaka ya kisiasa na kugeukia makosa ya jinai.
Aidha, limemtaka kuacha mara moja
kuihamasisha jamii, kutofuata sheria na taratibu za nchi, kwani nao atakuwa
anawaingiza matatani.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi ilitolewa jana na Kamishna wa Jeshi hilo anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi ilitolewa jana na Kamishna wa Jeshi hilo anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo Mbowe na wafuasi
wake, watafanya migomo na maandamano bila ya kufuata sheria, hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake, kwa kuwa tayari alishapewa onyo mara ya kwanza
kufuatia kauli hiyo.
Alisema Mbowe anatakiwa kufuata
taratibu na sheria kuhusu kufanya maandamano, kwani taratibu zote zipo, hivyo
kwa kauli zake hizo, anavunja sheria na kuvuka mipaka iliyowekwa kugeuka kuwa
jinai na siyo siasa.
‘’Kauli
iliyotolewa na Mbowe Septemba 14 (juzi) inaashiria uvunjifu wa amani na
inahamasisha jamii kutotii sheria na taratibu za nchi. Tunaonya kwamba Mbowe
anatakiwa kufuta kauli yake na kwamba taratibu zote zilizowekwa zifuatwe,’’ alisema Chagonja.
Awali, alisema kwamba siasa zina
mipaka yake, hivyo mtu atakayetumia mwavuli wa siasa kutaka kuvuruga amani na
utulivu uliopo, jeshi hilo halitamvumilia na halitasita kumchukulia hatua kali
kama mhalifu mwingine.
‘’Masuala
ya Bunge yana sheria na taratibu zake, hivyo kuna masuala mengine ya ndani
ambayo hayatakiwi kutolewa nje bila ya kufuata taratibu zilizowekwa na bunge
hilo, haikumpasa kusema kwamba atashinikiza wafuasi wake na wananchi kufanya
maandamano yasiyofuata sheria,’’
aliongeza.
Aidha, aliwaonya wananchi wote
kuzingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa katika kutekeleza jambo lolote,
pia kuepuka kauli zitakazowashawishi kuvunja sheria hizo.
Alisisitiza kuwa ili kuimarisha
amani na utulivu uliopo, wananchi wanatakiwa kutoshiriki katika masuala ya
uvunjifu wa amani kwa namna yoyote, badala yake kushiriki katika shughuli zao
za kulijenga taifa na kuleta maendeleo.
Wabunge wacharuka
Wakati Jeshi la Polisi likionya kuhusu kauli zinazotajwa kuwa za kichochezi za Mbowe, Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba nao jana waliibuka na kulishutumu kundi la wajumbe wa bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuhamasisha watu kuandamana barabarani, kupinga kuwepo kwa Bunge hilo huku viongozi wa kundi hilo wakionesha kuwa mstari wa mbele.
Wakati Jeshi la Polisi likionya kuhusu kauli zinazotajwa kuwa za kichochezi za Mbowe, Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba nao jana waliibuka na kulishutumu kundi la wajumbe wa bunge hilo wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kuhamasisha watu kuandamana barabarani, kupinga kuwepo kwa Bunge hilo huku viongozi wa kundi hilo wakionesha kuwa mstari wa mbele.
Wajumbe hao pia wameshutumu kitendo
cha Ukawa, kumwandama Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwa kufafanua
kwamba Bunge hilo, sio mali ya Sitta, bali linafanyika kwa mujibu wa sheria za
nchi.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba naye ameshutumiwa kuwa ndiye chanzo cha vurugu na
chokochoko, zinazoendelea kufanywa na UKAWA, kutokana na kauli zake, ambazo
amekuwa akizitoa kuwa Bunge hilo limepoteza uhalali wa kisiasa.
Akizungumza wakati wa majadiliano
bungeni, George Simbachawene alisema Ukawa wamekuwa wanafanya upotoshaji mkubwa
kwa kuutangazia umma kuwa uwepo wa bunge hilo sio halali. Alionya kuwa wananchi
sasa wanapaswa kupima uzalendo wa viongozi wa kundi hilo kupitia kauli zao.
Alisema Bunge hilo, sio mali ya
Sitta ambaye ni Mwenyekiti na kuwa kiongozi huyo na hata Rais, hana mamlaka ya
kulisitisha, kwani linaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Alisema kwa wingi wa wajumbe walioko
bungeni, hawawezi kuwa wendawazimu kuendelea na jambo ambalo sio halali.
Alisema kuwa wale ambao waliamua
kutoka nje ya Bunge hilo, ndio ambao wamevunja sheria. Simbachawene alisisitiza
kuwa wanachofanya wajumbe hao ni kupinga Katiba inayopendekezwa.
Alihoji; “Hivi kuingia barabarani kuandamana ndio kutunga Katiba ya wananchi?
Halafu hao Ukawa ndio wanataka tuwape nchi, kwa kweli naomba wananchi wawaone
kwamba watu hawa ni wabaya”.
Aliwahadharisha wananchi wasiende
kuandamana, badala yake wasubiri wapige kura ya kuikubali au kuikataa Katiba
hiyo na sio kwenda kuandamana.
Simbachawene ambaye pia ni Mbunge wa
Kibakwe na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alikiri kuwa
bunge hilo limewakosa walio nje kwa sababu waliwahitaji ili wachangie mawazo
mbadala, lakini wamekosa uzalendo kwa kukataa kurejea bungeni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi
Maalumu), Profesa Mark Mwandosya aliwashangaa Ukawa kuwachochea vijana
waandamane nchi nzima wakati viongozi wao hawashiriki maandamano hayo.
Alisema Chadema na washirika wake wa
Ukawa, wasiwapeleke vijana ambao ni tumaini la taifa hili kwenye maandamano,
kwani kufanya hivyo ni hatari kwa maisha ya vijana hao ambao ni nguvukazi ya
taifa.
Kapteni John Komba, yeye katika
mchango wake alitumia muda wake mwingi, kumshutumu Jaji Warioba, kuwa ndiye
aliyesababisha vurugu zote zinazoendelea nchini juu ya mchakato wa Katiba.
Alisema Jaji Warioba aliheshimiwa na
Rais Jakaya Kikwete na wananchi walimheshimu, ndio maana alikabidhiwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kwa ajili ya kukusanya na kuandika mabadiliko ya Katiba na
wakati huo Watanzania walikuwa kimya.
Alisema yeye baada ya kumaliza kazi
yake, kazi hiyo sasa ni ya Bunge Maalumu la Katiba, lakini kila kinachofanywa
na bunge hilo Jaji Warioba anawakosoa na alimwomba Mwenyekiti wa Bunge hilo,
atoe tamko la kumkemea mwanasheria huyo.
Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga
Magharibi, alishauri Jaji Warioba akae kimya katika kipindi hiki ambacho bunge
hilo linamalizia kazi yake ya kuandika katiba hiyo.
Komba pia alimshutumu Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe kwa kujigeuza kuwa Amiri Jeshi kwa kutangaza vita na
kuwataka wafuasi wake waingie barabarani nchi nzima katika maandamano ambayo
hayana kikomo.
“Si
mlimsikia akisema ‘mko tayari kwa vita?’ Wakamjibu ‘tuko tayari’…akaendelea,
‘lakini mjue kuna risasi mko tayari’ na wafuasi wake wakajibu ‘ndio tuko
tayari’… hivi hii ni amani gani wanayoitangaza huko nje, hii ni hatari kwa
nchi,” alisema Komba.
Amos Makalla, mjumbe na Mbunge wa
Mvomero ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, aliungana na wajumbe wengine,
kuwashambulia Ukawa bungeni. Alisema kuwa umoja wao huo, maana yake ni umoja wa
katiba ya wachache na sio ya wananchi, kama wanavyojitangaza.
Alisema kama ingekuwa ni umoja wa
katiba ya wananchi walio wengi, kundi hilo lingebaki ndani ili waandike na
kushiriki kwenye mambo yanayogusa wananchi wao ;na sio kutoka nje ya Bunge.
Alimtaka Sitta asitishike na kauli
za Ukawa, badala yake awe imara ili kazi iliyobaki ya kuandika Katiba ya nchi
imalizike.
Mwenyekiti wa Chama cha UPDP, Fahmi
Dovutwa aliliambia bunge hilo kuwa wenzake hao wa upinzani, wanamsakama Sitta
kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao wakati wa mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa
bunge hilo.
Alisema wakati wa mchakato wa
kumchagua mwenyekiti, vyama vyote vya upinzani venye wabunge ambavyo vinaunda
Ukawa, walimuunga mkono Sitta kwa mategemeo kuwa angelinda maslahi yao.
Mwanasiasa huyo ambaye mara nyingi
amekuwa anatofautiana na misimamo ya Ukawa tangu bunge hilo kuanza, alisema
waliamini kuwa Sitta angewaunga mkono katika hoja zao za ovyo, ambazo alidai
hazina faida kwa nchi, ndio maana wanamshambulia kila kukicha.
Mohammed Misanga alimtaka Sitta
asitetereke kwa kuitwa king’ang’anizi, kwani wananchi walio wengi wanaliunga
mkono bunge hilo, kutokana na mambo mengi yanayojadiliwa kuwahusu wao.
“Nimeongea
na wananchi kwenye jimbo langu na kule Dar es Salaam wanawashangaa hawa Ukawa,
maana haya mambo tunayozungumzia hapa ni ya wananchi wenyewe,” alisema Misanga ambaye pia ni Mbunge wa Singida Magharibi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment