Mkutano huu
ambao ni wa kitaalamu unawakutanisha
wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo,
wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango ambao hukutana kwa ajili ya
kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa
masuala ya maendeleo ya kitaaluma.
Mkutano huu unatoa
fursa kubwa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa
pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Pia hutoa fursa za
kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa
kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. Mkutano huo ni muhimu katika
kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo
ya kiuchumi na kijamii nchini.
Kwa kutilia
mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, mkutano wa
mwaka huu utajikita katika kujadili masuala yafuatayo;
i) Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango
(wachumi, maafisa mipango na watakwimu);
Mkutano
utajadili fursa, na changamoto zilizopo katika kuleta maendeleo katika nchi. Huko nyuma kada hizi zilikuwa zinaratibiwa na iliyokuwa
Wizara ya Mipango Uchumi na Uwezeshaji. Kwa sasa watakuwa chini ya uratibu wa
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Hatua hii itarahisisha utekelezaji wa mipango
mbalimbali ya nchi.
ii) Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo
wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021);
Utekelezaji wa
Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16) unaendelea na tayari
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango imeanza kufanya mapitio ya utekelezaji wake ili
kujua mafanikio na changamoto. Hivyo, katika mkutano huo wapanga mipango
wanaandaliwa waweze kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Mpango wa Pili wa Maendeleo
(2015/16 – 2020/21).
iii)
Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma;
Serikali
imeandaa mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika sekta ya Umma, lengo likiwa
kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za
umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo.
iv)
Jinsi ya Kujiandaa na Uchumi wa Gesi
Mkutano
utajadili ni kwa jinsi gani Tanzania inajipanga kufaidika na rasilimali ya gesi
asilia. Kwa kifupi masuala ya yanayohusu uwekezaji katika gesi asilia,
usimamizi na jinsi ya kutumia rasilimali na menejimenti ya mapato yatokanayo na
gesi, pamoja na ushiriki wa wananchi katika fursa mbalimbali zinazotokana na
ujio wa gesi hiyo. Utayarishaji wa wataalam katika eneo hilo la gesi husani
vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na kadhalika.
Washiriki wa mkutano
huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye
wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za
kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Mkutano wa
mwisho wa mwaka wa maafisa mipango ulifanyika mkoani Morogoro tarehe 12 Machi
2010 ambapo uliandaliwa na Wizara ya Fedha.
Mada nne zilizowasilishwa na kujadiliwa zilikuwa
ni;
i.
Wajibu wa wataalamu wa mipango katika Maendeleo ya Uchumi:
Mipango ya Kiuchumi, Utekelezaji na Uandaaji wa Taarifa;
ii.
Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki;
iii.
Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara
kwa Wafanyabiashara Wadogo na Wakati; na
iv.
Ufanisi wa Uwekezaji kutoka nje katika Uchumi
wa Tanzania
Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment