Rais Braise Compaore wa Burkina Faso ametangaza kujiuzulu nafasi yake muda mfupi.
Tangazo hilo limetolewa na jeshi la nchi hiyo ambalo ndilo linashikilia nafasi kwamuda huu.
Na Mwanaharakati.
Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Friday, 31 October 2014
ASKARI POLISI ASHIKILIWA KWA KUMKATA MFANYAKAZI WAKE VIDOLE VINNE KWA PANGA
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma
wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi
wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga,
akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake.
Tukio hilo la kujeruhiwa kijana
Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji
cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao
kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake
nyumbani eneo la Igogo.
Kijana huyo alieleza kuwa kufanya
kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na
kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili
kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/=
kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa
muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.
“Nilipoona hajanilipa mshahara wangu
kwa muda wa miezi sita huku kila ni kimwambia ananijia juu na kunitukana matusi
basi nilimuomba ruhusa ya kwenda kijijini Oktoba 15 mwaka huu kumuona mama
yangu mzazi aliyekuwa anaumwa ili kupata nafasi ya kurudi nyumbani” alisema.
Steven alieleza kuwa wakati akiwa
kijijini askari huyo (Mwajili wake) alikuwa akimpigia simu kumtaka arudi Mwanza
kuendelea na kazi na kudai kuwa atamlipa malimbikizo ya mshahara wake kiasi cha
Sh 300,000/= zilizokuwa kama deni, Steven alikubali ombi hilo kwa kuomba
atumiwe nauli na pesa kidogo ya kumwachia mama yake, jambo ambalo askari huyo
alikaa kimya bila majibu.
“Siku ya Oktoba 20 mwaka huu majira
ya saa 4:00 asubuhi alifika kijijini akiwa na askari watatu kwenye gari la
Polisi (Difenda) wa Kituo cha Mugumu na kudai kuwa nipo chini ya ulinzi kisha
kunifunga pingu, akidai kuwa nilimwibia Deki ya Video na kutoroka nyumbani
kwake, walinipandisha kwenye Difenda kunipeleka kituoni “ alisema.
Kijana huyo alieleza kuwa baada ya
kufikishwa kituoni Mugumu askari huyo na wenzake walianza kumuhoji huku wakimpa
maneno ya vitisho, kijana huyo alipokataa kuwa hakuiba wala kutoroka, Sajenti
Fatuma aliamuru kijana huyo kuvulishwa shati alilovaa na kisha akafungwa usoni
na kuombwa anyooshe mkono mezani ili apewe 'Sapraizi'.
"Sekunde chache nilihisi kitu
kikali kimenipitia kwenye vidole vyangu vinne vya mkono wa kulia na kufuatiwa
na maumivu makali, niliusogeza mkono wangu mdomoni kuupoza kwa kuupuliza ndipo
nilipo gundua kuwa nimekatwa kabisa vidole vyangu vinne vya mkono wangu wa
kulia ikibakia dole gumba tu" kijana Steven alisimulia kwa uchungu.
“Niliangua kilio kutokana na maumizu
na sijui vidole vyangu hadi sasa sijui vikowapi, askari wenzake baada ya kuona
nimetokwa na damu nyingi walimshauri anipeleke hospitali ya Wilaya ya Mugumu
ili nipatiwe matibabu kabla ya kuondoka kuja Mwanza,”alisisitiza.
Steven alisema baada ya kupatiwa
matibabu, tulienda kupanda basi ili kuja Mwanza kwa madai kuwa amenifungulia
kesi ya wizi wa Deki ya Video na tuliopfika alinipeleka kituo cha Polisi Kati
Nyamagana na kuniweka Mahabusu akinituhumu wizi, lakini nilipochukuliwa maelezo
nilikana tuhuma za wizi na kueleza ukweli wangu ili kupata msaada.
Huku taarifa zingine kutoka ndani ya
jeshi zilizopatikana zilidai kuwa askari huyo alikusudia kufanya ukatili huo
kutokana na udanganyifu ambao alifanya kwa uongozi wake akiomba kupatiwa silaha
(SMG) kwa ajili ya kuitumia kwenye kazi za nje lakini lengo ikiwa ni kwenda na
silaha hiyo kwa ajili ya kumkamata na kumtishia kijana huyo, jambo ambalo
uongozi ulimgomea.
JESHI LA POLISI LINASEMAJE
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mwanza (RPC), Valentino Mlowola, jana ofisini kwake amethibitisha kuwepo kwa
taarifa za tukio hilo na kueleza kuwa tayari Jeshi hilo limechukuwa hatua
madhubuti hatua ya awali ikiwa ni kumshikilia askari huyo kwa kufanya ukatili
huo kwa kuvunja sheria na kujichukulia sheria mkononi kumjeruhi kijana huyo.
Mlowola alisema pamoja na kijana
huyo awali kufunguliwa jarada la kutuhumiwa kufanya kosa la wizi (Jinai) na
kudaiwa kutorokea kijijini kwao, bado askari huyo alitakiwa kufuata mfumo wa
kiutawala na kisheria uliopo kushughulikia suala hilo badala ya kuamua
kujichukulia maamuzi ya kumwadhibu mtuhumiwa kabla ya uthibitisho wa mashitaka
yaliyokuwa yamefungulia.
“Nilipopokea taarifa hizi kwa
mashangao na masikitiko makubwa na zimenisitua sana, si kitendo cha kiungwana
hata kidogo kwa mtu ambaye anatakiwa kufuata taratibu za mfumo wa utawala na
sheria katika utekelezaji wa kushughulikia kero na matatizo ya jamii, alitakiwa
kutumia busara kwani tayari aliishamfungulia jarada la kumtuhumu kumwibia
ikizingatiwa naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua
uchungu,”alisema.
Kamanda Mlowola alieleza kufatia
ukatili huo kufanywa na askari wake ameunda timu ya kikosi cha askari kwenda
hadi kijijini Magange wilayani Serengeti mkoani Mara ili kufanya uchunguzi wa
tukio hili ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano na familia, wananchi wa kijiji
hicho kisha Hospitali ya Wilaya ya Serengeti alipopatiwa matibabu ya awali.
“Ili tupate ukweli wa jambo hili
tumeunda timu hiyo, kwani kijana Steven tumemhoji ametueleza jinsi askari
Fatuma alichomfanyia na kudai hakumwibia, lakini askri wetu pia amehojiwa awali
amedai hakufanya kitendo hicho bali wananchi ndo walimfanyia ukatili huo hivyo
ni mkanganyiko lakini ukweli utapatikana tu japo kuwa tukio hili halikufanyika
Mwanza”alisisitiza.
Mlowola alisema kwamba tayari
tunamshikiria askari huyu na kumfungulia jarada la uchunguzi kwa taratibu za
kijeshi na ikibainika kutenda kosa hilo tutumfukuza kazi na kumfikisha katika
vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua zaidi kulingana na kosa alilofanya,
lakini pia kijana Steven naye anashikiriwa kwa tuhuma alizonazo za wizi kufatia
jarada lililopo.
“Hatuwezi kuendelea kucheka na
kufumbia macho kitendo hiki ni jambo ambalo linamgusa kila mtu hata mimi ni
mzazi ukiachana na utumishi wangu wa umma, ntahakikisha jambo hili
nalishughulikia kwa umakini na kutoa taarifa kwa umma ili pia kueleza wananchi
kuwa tukio hili limefanywa na mtumishi kama mtu si Taasisi ya Jeshi la Polisi
na ahidi kutenda haki kwenye hili,”alisisitiza.
Wito wangu kwa wananchi ni kuacha
kujichukulia sheria mkononi na kuwaadhibu watuhumiwa mbalimbali kabla ya
kuthibitika kwa makosa na tuhuma hizo, lakini wazingatie kufuata taratibu za
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili kushughulikia matatizo yao nawaomba waendelee
kutoa ushirikiana na kufuata mfumo uliopo badala ya kujichukulia sheria
mkononi.
NaG.SENGO
Thursday, 30 October 2014
WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI OMAN
Baadhi ya watanzania waishio Oman wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo PInda wakati alipowahutubia kwenye hoteli ya Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu) |
ASKOFU ASHTUSHWA NA MAUAJI – GEITA
Na Valence Robert Geita.
WANANCHI Mkoani Geita wametakiwa
kuacha mara moja tabia ya kuwaua vikongwe kwa imani za kishirikina
na kuacha kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya hivyo wanakwenda kinyume
na mapenzi ya Mungu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Asikofu
wa kanisa la Habari Njema, Tryphone Siku, wakati wa kufungua mkutano wa siku
tano katika viwanja vya shule ya msingi kalangala vilivyoko mjini hapa. Lengo
likiwa ni kuwaombea watu kuacha dhambi na kumrudia mwenyezi Mungu.
Tryphone alisema kuwa watu wa Mkoa
huo wamekuwa wakiwaua vikongwe kwa imani za kishirikina na kujichukulia sheria
mikononi kwa kuwauwa wahalifu hivyo kuwaomba kuacha mara moja kwani wanakwenda
kinyume na mapenzi ya Mungu na kuwataka, waganga wanaopiga ramli chonganishi
nao kuacha.
Aliendelea kusema kuwa
viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa
huo Said Magalula wamekuwa wakijitahidi sana kuwaelimisha wananchi kuacha tabia
hizo kwa kushirikiana na makanisa likiwemo kanisa lake.
Naye Mchungaji wa kanisa hilo Alex
Mshindi kutoka Rwanda alishukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano
huo lakini akawaomba wakazi wa Mkoa wa Geita kwa ujumla kuwa wanatakiwa
kumrudia aliyewaumba na kuacha matendo maovu.
Nimeshangazwa na mauaji ya vikongwe
na kujiochukulia sheria mikononi ninavyosikia hapa Mkoani kwenu
jamani acheni tabia hizo lakini tushirikiane kuwaombea wanaofanya hivi waache
na wamrudie muumba wao. Alisema Alex.
Na Mwanaharakati.
BREAKING NEWS!!! KIFO CHA MSANII MKONGWE BONGO MOVIE
Habari zilizotufukia hivi punde zinasema kuwa muigizaji Mzee Manento amefariki dunia hapo jana. Bado tunafuatilia kwa karibu habari hizi za chanzo cha kifo cha mzee wetu huyu.
Mzee Manento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakini na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
Na Mwanaharakati.
TAZAMA PICHA ZA KUSIKITISHA AJALI ILIYOUA WATU ARUSHA
Akiongea na mwandishi wetu, mmoja ya mashahidi
aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru, amesema ajali ilitokea
majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani –Tengeru jana iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace
linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.
Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace
(gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso
kwa uso na lori hilo. Na Mwanaharakati.
Subscribe to:
Posts (Atom)