Kijana huyo mkazi wa Ilboru,
alihukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 70 akidaiwa kutenda kosa la
kumshambulia baba yake mzazi aliyetambulika kwa jina la mzee Ng’uraa na
kumng’oa jino moja.


Hiyo ni
kupitia sheria iliyopitishwa na wakazi wa Arumeru
mkoani Arusha ya kuwachapa viboko 70 hadi 120 wasichana wanaovaa nusu uchi na
wavulana wanaovaa mlegezo, kuvuta bangi, wizi, matusi na ulevi nyakati za kazi
imeanza kufanya kazi baada ya kijana Zakayo Leonard (26) kuchapwa viboko 120
kwa makosa mbalimbali likiwemo uchafu wa kutofua nguo zake.
Pia alitandikwa viboko 30 kwa kosa
la kumtolea maneno machafu mzee wa kimila (Laigwanani) na baadaye alicharazwa
viboko 20 kutokana na tabia ya uchafu wa kutofua nguo zake.
Hata hivyo, mara baada ya adhabu
hiyo ya viboko 120 kwa mkupuo, kijana huyo alizimia na kushindwa kuinuka wala
kutembea hali iliyolazimika kusaidiwa kwa kubebwa na morani wa Kimasai hadi
nyumbani kwake.
Adhabu hiyo ilitekelezwa hadharani
mbele ya wazee wawili wa ukoo (Laigwanani) waliokuwa wakishuhudia huku
mtuhumiwa akitakiwa kutojigusa popote wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo na
kwamba iwapo angejishika popote viboko hivyo alivyochapwa vingefutwa na kurejea
upya.
Wazee wa makabila ya Wamasi,
Waarusha na Wameru wamejiwekea utaratibu wa kimila bila kujali kama unafuata
maadili ya mwanadamu kwa kuwaadhibu wahalifu hadharani bila kuwafikisha kwenye
vyombo vya sheria.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment