
![]() |
Bw Wiliam Rutta akihutubia wageni na wahitimu shuleni Tweyambe |

Wazazi na walezi mkoani Kagera, wameshauriwa kuendelea
kuwawekea mazingira bora ya elimu watoto wao kutokana na mabadiliko ya kiwango
kizuri cha elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Tamim Kassi Suleiman katika mahafali
ya shule ya sekondari Tweyambe wilayani Misenyi, akisisitiza kuwa kiwango cha
kidato cha nne saizi hakiwezi kumletea muhitimu maendeleo kama hajajiunga
kidato cha tano.
Amesema kuwa zamani aliyekuwa akimaliza kidato cha nne,
angeonekana mtu mkubwa kwenye jamii kwasababu alifanikiwa kupata kazi sehemu
yoyote, tofauti na sasa ambapo kila kazi inahitaji kiwango cha juu hivyo
kutakiwa kuwa na elimu ya juu.
Mgeni rasimi katika mahafali hayo Bw Wiliam Rutta, amesema
kuwa ni lazima elimu itengenezewe mazingira mazuri ili kuleta mafanikio, hivyo
kama mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo, atahkikisha anaedeleza mawasiliano
ya kuitangaza shule hiyo, huku akisema kuwa kwa kushirikiana na wahisani
mbalimbali anaofanya nao kazi, watajitaidi kutatua tatizo la maji na masuala ya
michezo shuleni hapo.
Wakati huo huo amewataka wazazi kutunzafedha kidogokidogo
ili kiwasaidie kusomesha watoto pasipokutegemea misaada pekee.
Shule hiyo ya
sekondari Tweyambe, ina jumla ya wanafuzi wa kike na kiume 521, wakiwamao wa
bweni 410 na 111 wa kutwa, ina walimu 22
ambao 19 wa kiume na 3 wa kike
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment