MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 7 December 2014

ALICHOSEMA KOCHA KIBADEN BAADA YA MITANDAO KUMZUSHIA KIFO JANA

 


Taarifa ziliripotiwa na mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara.

“Kweli hata mimi napigiwa simu na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi taarifa.

“Kweli siku chache zilizopita nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata gari.

“Kupitia mtandao wako, naomba niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.

“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: