Mgombea Uenyekiti kupitia Chama cha
CCM Mtaa wa Swea kata ya Mkolani Mwanza Pius Mihayo amefariki dunia gafla akiwa
mtaani kwake muda mfupi baada ya kupiga kura.
Msimamizi wa uchaguzi huo Halifa
Hida alisema mgombea huyo alifariki dunia gafla akiwa kwenye mtaa wake wa Swea
na chanzo cha kifo chake hakijajulikana.
“Sasa kwa mujibu wa taratibu za
uchaguzi,tutatangaza matokeo ya wajumbe na nafasi za wagombea wa
vitimaalum,nafasi ya uenyekiti haitatangazwa hadi taratibu nyingine za uchaguzi
zitakapoandaliwa”alisema Hida.
Mkoani Arushamsongamano wa
wapigakura katika kituo chaMbauda kata ya Sombetini unadaiwa kusababisha kifo
cha mtu aliyetambulika kwa jina la Suleiman Bakari.
Tukio hilo lilitokea saa 3 asubuhi
katika kituo hicho ambacho kilikua kimefurika watu ambapomtu huyo alianguka
gafla baadaya kukosa hewa akiwa kwenye mstari wa kupigakura.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment