MWANAMUZIKI mkongwe mwenye umahiri
wa kuimba na kucharaza gitaa kiongozi la Solo, Shem Ibrahim Karenga amefariki
dunia leo akiwa katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alipokuwa
akitibiwa.
Wengi wanamfahamu Shem
Karenga kupitia tungo zake mbalimbali zilizochangia kumpa umarufu,
alizozifyatua akiwa na bendi hizi na zile, kama vile ‘Tucheze Segere’, ‘Muna’,
‘Kila jambo’ na ‘Mbelaombe’.
Shem Karenga alizaliwa mwaka 1950, Bangwe, Kigoma na
kupata elimu ya msingi katika shule ya kimishionari ya Kihezya kuanzia mwaka
1957 hadi mwaka 1964.
Mwaka 1964 alijiunga na bendi ya Lake Tanganyika
Jazz ambayo maskani yake yalikuwa mjini Kigoma. Mwaka 1972, aliitwa kwenye
bendi ya Tabora Jazz kama mwanamuziki mwenye kipaji cha utunzi, mwimbaji na
mpigaji wa gitaa la Solo.
Mwaka 1983 alijiengua kutoka Tabora Jazz na kusimama
kabisa kujihusisha na muziki, ambako kilichofuatia ilikuwa ni kifo cha bendi
hiyo. Mwaka 1990 aliondoka Tabora na kutua jijini Dar es Salaam. Mwaka 1990
alijiunga na MK Beats. Mwaka 1995, MK Beats ilisambaratika, ambako mwaka
uliofuata, yaani 1996 alianzisha bendi ya Tabora Jazz Star kwa kushirikiana na
Ibrahim Didi.
Mpaka mauti yanamfika, Shem Karenga Mkurugenzi
Msaidizi katika Bendi ya Tabora Jazz Star ambapo Mkurugenzi Mkuu ni Ibrahim
Didi. Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Shem Karenga anatarajiwa kuzikwa
kesho.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI ANAPOSTAILINa Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment