MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 14 December 2014

MATUKIO MAPYA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


 Kutoka Ulanga mkoaniTabora, wananchi hawajapiga kura kwasababu ya vifaa kuchelewa ambapo wananchi katika vituo386 bado wamesubiri hadi sasa saa 7 mchana.
Kituo Mkituli Kibeta anakoishi Wilfred Rwakatare, hadi saa 5kura zilikuwa hazijapigwa sababu ya mkanganyiko uliotolewa baada ya mgombea CCM kutoa na baadaye akajirejesha huku uratibu haukurudisha jina lake, baadaye walikubaliana kuwa wapige kwa kumpigia mgombea aliyepo kwenye karatasi.

 
Kituo cha Kibeta Akiumura,hapa wapo makada wa vyama mbalimbali  wanaopokea kilaanayekuja kwa kisingizokuwa hawajui kuandika, nawanawapelekakuwaandikia,
 



Kituo hikiniKashaiKashenye ambapo ni katikakiwanja chakanisa wakati ibaada zikiendelea, wapiga kura wakikumbana na kelele za kwaya.
Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana


Kutoka Songea Mjini, kata ya Misufini hadi sasa kura hazijaanza kupigwa kwa sababu fomu za kupiga kura nafasi ya uenyekiti wa mtaa zimechanganywa, kwani kwenye nembo ya CCM jina lililoandikwa ni la mgombea wa CHADEMA kama inavyoonyesha kwenye picha.

Na Mwanaharakati.

No comments: