Maji hayo yanaweza kuhatarisha maisha ya watu kutokana na uchafu huo ambapo watoto upendelea kuogelea katikamaeneo kadhaa ya ziwa hilo.
UCHAFUZI wa mazingira kwa maeneo
yanayozunguka shughuli za uchimbaji madini ukiwemo mgodi wa dhahabu wa Geita
Gold Mine(GGM) hautaisha endapo jamii haitashirikishwa na wenye makampuni
wanaoendesha shughuli za kimadini ambao pia ni vyanzo vya uchafuzi huo.
Aidha mji wa Geita unaozungukwa na
shughuli za uchimbaji kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya athari za
kimazingira jambo ambalo watu mbalimbali wamekuwa wakifika kufanya tafiti
tofauti ili kubaini madhara ya athari hizo zinazoongelewa kila mara katika
jamii.
Mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe
kitivo cha sheria Hanifa Massawe amekuwa miongoni mwa watafiti wa uharibifu wa
mazingira katika mji wa Geita kutokana na shughuli za kimadini zinazoendelea
kwa mda mrefu bila kuzipatia majawabu kwa jamii.
Baadhi ya sababu alizokutana nazo
wakati wa tafiti hiyo ni pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji
yanayotumika,uchafuzi wa aridhi katika ulipuaji wa miamba kwa wachimbaji
wakubwa na wadogo waliopo maeneo ya samina,Mponvu,mgusu na Nyakabale maeneo
ambayo uchimbaji upo kwa wingi.
Hivyo mhadhiri huyo ameshauri kuwa
changamoto hizi zitafutiwe majawabu na mamlaka husika kwa wakati kwani huenda
hazitafutiwi ufumbuzi kutokana na mamlaka zinazohusika kutotilia mkazo mambo
hayo lakini pia mamlaka hazifuatilii kwa karibu matatizo hayo.
Wakati huohuo katibu wa kituo cha
sheria na haki za binadamu wilaya ya Geita Elineema Mafie amesema kuwa
hari ya mahusiano kati ya wachimbaji na wananchi hususani mgodi mkubwa wa GGM
siyo ya kuridhisha kiasi kwamba ukuikwaji wa haki za binadamu unajitokeza sana
na upo kwa mda mrefu bila kuupatia ufumbuzi wake.
Ameongeza kuwa kumekuwa na mahusiano
kati ya mgodi na viongozi wa mitaa hususani wenyeviti wakiwa na vikao vya
mahusiano lakini cha ajabu wenyeviti hao hawarudishi majibu kwa wananchi ambao
ndio wahanga wa matukio hayo hivyo ametaka kuwepo utaratibu wa wenyeviti kukaa
na wananchi ili kuwapa mrejesho juu ya mahusiani wanayofanya mgodi.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment