Aliyekuwa Shehe Mkuu wa Bakwata
Wilaya ya Mbeya, Abubakar Mketo amefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita
kufuatia kuanguka ghafla makaburini wakati akitoa mawaidha ya Kiislam ya jinsi
waumini wanavyotakiwa kuishi katika ulimwengu wa dhambi! Inauma sana!
ILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo, baada ya kumaliza kuusitiri mwili wa marehemu Bibi Majuto ndani ya nyumba
yake ya milele, Shehe Mketo alisimama na kuanza kutoa mawaidha kwa waombolezaji
waliohudhuria mazishi hayo akiwaelekeza namna ya kuishi kwa kutii amri za Mungu
na kufuata njia zake kwa vile hakuna anayejua atakufa lini kama ilivyokuwa kwa
marehemu Bibi Majuto.
MANENO YAKE YA MWISHO
Vyanzo vinadai kuwa, dakika chache
kabla ya shehe huyo hajapatwa na mauti alionekana ni mwenye afya njema huku
akitoa Neno la Mungu ambalo kila mtu aliyekuwa eneo hilo la makaburi lilimgusa
na kujitafakari upya njia zake, alisema
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment