Askari wa Kikosi cha Zimamoto na
Uokoaji akishuka baada ya kumuokoa mtoto eneo la Mabatini, jijini Mwanza
lililokumbwa na mafuriko baada ya Mto Mirongo kufurika kutokana na mvua
iliyonyesha jana. Picha na Michael Jamson
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Mbugani,
Mtaa wa Mbugani A na B wameathiriwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa
iliyonyesha jana kwa saa nne.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
wakazi hao walisema mvua hiyo imesababisha vitu vyao kusombwa na maji na nyumba
kubomoka.
Esther Misanga, mkazi wa mtaa huo,
alitaja baadhi ya vitu vilivyoharibiwa na mvua hiyo kuwa ni magunia 20 ya
mahindi, magunia 10 ya daga na mifuko 20 ya unga wa sembe, vyote vikiwa na
thamani ya jumla ya Sh2 milioni.
“Nimepoteza magunia 50 ya mahindi na
unga wa dona. Nimepata hasara kubwa sana. Sikutegemea yangetokea mafuriko
makubwa kama haya,” alisema Misanga.
Alisema Serikali iliwaahidi
kuwahamisha maeneo hayo kutokana na kupata adha ya mafuriko ya mara kwa mara,
lakini hadi sasa utekelezaji huo haujafanyika.
“Serikali ilituahidi kutupatia
maeneo kule Kisesa, lakini tangu wazungumze hadi sasa mwaka umepita
hawajatuonyesha maeneo hayo. Tunaiomba Serikali ifanye kila liwezekanalo
ituhamishe katika eneo hili tunusuru maisha yetu,” alisema Misanga.
Akizungumza kwa simu, mtendaji wa
Kata ya Mbungani, Baruani Hawadhi alisema maafa hayo siyo makubwa kwa kuwa
hajapata taarifa za vifo vya watu zaidi ya uharibifu wa mali za watu
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment