MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 6 January 2015

PICHA NA TAARIFA ZA BABA KUMTOBOA MTOTO MACHO NAYE KUJINYONGA KAGERA SOMA HAPA

Godfrey Joseph Kajuna (45miaka)

Ni Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) alikuwa mkaazi katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera amejinyonga hadi kufa baada ya kumfanyia ukatili mtoto  wake wa kuzaa.

Inasemekana kuwa baba huyo alimpiga na kumjeruhi kichwani kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mwanae  aitwaye Agripina Godfrey (12) anayesoma darasa la Kwanza katika shule ya msingi Ilambika. 

Taarifa za awali zisizo rasmi zinasema Baba alitoka ndani na kuwaambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango, ndipo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kumfungulia Mlango.

Mama akaondoka kujiifadhi sehemu.
Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto aliyeonekana kama ndiyo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa "Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba yake aanze kumpiga sana! Mpaka kumuumiza vile.


Damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani na alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe.

Mtoto alipelekwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.

Na Mwanaharakati.

No comments: