
Mwalimu Gaudencia Gitano (40) anayefundisha Shule ya Msingi Kivelu jijini Dar es Salaam, amedai huenda yeye ndiye anayeongoza kwa kupigwa kuliko wanawake wengine wote jijini, baada ya kudai anazo RB tano za vipigo tofauti kutoka kwa mumewe kwa nyakati mbalimbali tangu aolewe Oktoba 25, 2002, katika ndoa ya kiserikali iliyofungwa Ilala Boma.
Akizungumza akiwa kitandani katika Hospitali ya Dar Group iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Gaudensia (pichani), alidai kupigwa mara kwa mara kiasi kwamba katika vituo vya polisi na hospitali, amekuwa ni mwenyeji.
“Mimi ni mke wa pili kati ya watatu na tulifunga ndoa ya kiserikali na mume wangu Colman Marwa Oktoba 25, 2002 huko Ilala Boma.
Tulikuwa tukipendana na Mungu ametujaalia tumepata watoto wawili, tulikuwa tukiishi pamoja katika nyumba yetu huko Kitunda na baadaye tukahamia katika nyumba yetu nyingine huko Msongola.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment