MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 16 February 2015

TAARIFA YA KISIWA KILICHOKUMBWA NA KIMBUNGA,MSAADA WA MAMILIONI WAHITAJIKA



Kaya 76 zinaishi bila makaazi, huku shilingi milioni 137 zikiitajika ili kunusuru maisha ya wakaazi 122 wa Kaya hizo.

Shilingi milioni 137 zinahitajika kukarabati majengo na miundombinu mbalimbali katika kisiwa cha Goziba wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya kisiwa hicho kukumbwa na kimbunga na kusababisha madhara  kwa wananchi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Goziba Bw Leonard Mapesa, amesema.......
kuwa mpaka sasa wananchi waliothiriwa zaidi, wamepata msaada wa shilingi laki tisa na nusu kutoka wilaya ya Muleba ili wanunue maidi ya chakula, msaada mwingine wa wilaya hiyo ni vyandarua 80 na blancket 30.

Hatahivyo Bw Mapesa amesema kuwa mbunge wa Muleba kaskazini Bw Caharles Mwijage, ametoa shilingi milioni moja na laki mbili kwa ajili ya majeruhi zaidi ya therathini waliokuwa wamelazwa hospitali ya mkoa wa Kagera. 

Ameongeza kuwa baadhi ya wananchi wameweza kurudishia nyumba zao kidogokidogo, huku wengine wakishindwa kutokana na uwezo mdongo, huku akisema kuwa hali ya uchumi ni mbaya kutokana na msimu wa samaki kutokuwa mzuri, hivyo wananchi wanategemea msaada wa wahisani ili waweze kujijenga upya, ilhali wakiofia kupoteza maisha kutokana na njaa inayowakumba wakaazi hao.

Akielezea hali ya kiwa cha Goziba, mkuu wa wilaya ya Muleba Bw Lebris Kipuyo, amesema kuwa asilimia 95 ya nyumba zilizokuwa zimejengwa kisiwani humo ziliwa za mabati yaani FULL SOUITE, hivyo wakati wa mahafa tarehe 29 januari 2015, mabati hayo ndiyo yalisababisha wananchi wengi kujeruhiwa huku, watatu wakipoteza maisha. 

Ameongeza kuwa wanashindwa kujenga majengo ya tofari kutokana na mchanga wa eneo hilo, hivyo serikali pamoja na wahisani wenye uwezo, wanaombwa kujitokeza kusaidia wakaazi wa Kisiwa hicho ili wawe na makaazi bora ambayo hayawezi kusababisha madhara makubwa kama ilivyotokea.

Mkuu huyo wa wilaya, amewataka wakaazi Goziba kilichopo umbali wa kilomita 80 kutoka Wilaya ya Muleba kutopenda kuingia hewani bila kuhakiki hali ya hewa, huku akizitaka kamati za ulinzi na usalama kusimamia mali za wahanga ili zisiibiwe kwani wengi hawana pa kuivadhi michango inayotolewa.

Kisiwa cha Goziba, kina wakazi zaidi ya elfu saba, ambao wanategemea shughuli za uvuvi ila kwasasa uzalishaji umekwama kutokana na uharibifu wa vitendea kazi vyao pamoja na msimu wa samaki kuwa mbaya kwa kukosa samaki wa kutosha, huku wakikabiliwa na huduma za afya kutokana na kukosa wa hudumu na dawa ambavyo wanasema havitokani na kimbunga bali hawaja[ata huduma hizo japo wamejengewa kituo cha afya.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: