MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 19 February 2015

WADAU WA PAMBA SASA WASHUKIWA GEITA



WADAU wa sekta ya kilimo cha pamba wameshauriwa kutoa elimu ya kilimo cha pamba kwa wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji.

Wito huo umetolewa  jana na mwakilishi wa Mkuu wa.....
wilaya ya Geita Sashisha Masie  ambaye pia ni kaimu katibu tawala wa wilaya,  katika semina ya mafunzo kwa wadau wa zao hilo ambapo aliwata wadau hao wajikite zaidi katika kutoa elimu kwa wakulima umuhimu wa zao la pamba.

“Wito wangu kwenu mkitoka hapa mkawaelimishe wakulima wa zao la pamba umuhimu wa zao hili na jinsi ya kuzalisha kwasababu tumeshuhudia uzalishaji  wa zao hili umeshuka sana kutokana na wakulima wenyewe kutolisamini zao lenyewe namatumaini kwamba mafunzo mliopata yatakuwa ni mkombozi kwa wakulima,”alisema Masie.

“Pamba ni zao muhimu sana ni zao la biashara hivyo wakulima wakielimishwa vya kutosha na kupewa mafunzo ya kilimo bora ya zao hili naamini wakulima watalipenda na kulithamini kokote duniani pamba inategemewa kwasababu inamatumizi mengi,”alongeza Masie.

Naye Meneja mafunzo Joseph Tuku kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la Tanzania Gatsby Trust (TGT) linaloendesha semina hiyo, alisema kuwa shirika lao limejikita kutoa semina ya mafunzo ya pamba katika wilaya za Sengerema, Nyang’hwale na Geita.

Pia Tuku aliitaka serikali iungane na shirika la TGT katika utoaji wa elimu na ushauri kwa wakulima wa pamba.

Kwa upande wake Monica Jumbe ambaye ni mdau na mkulima wa zao hilo alisema amenufaika na mafunzo hayo kwani hivi sasa ameona umuhimu wa zao hilo pia alisema atakuwa wakala mzuri wa kuelimisha wakulima wengine.
                                          

Na Mwanaharakati.

No comments: