MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday 13 March 2015

WIZARA YA NISHATI YACHARUKIA WATOA LESENI ZA MADINI YA UJENZI, SOMA AGIZO LA WAZIRI HAPA MKOANI GEITA



Waziri wa  Nishati na madini nchini Mh. George Chawene amewaagiza maafisa madini nchini kote kuacha kutoa leseni za madini ya ujenzi kwa mtu mmoja mmoja badala yake watoe leseni hizo kwa vikundi au vijiji ili kurudisha mahusiano mazuri kati ya wananchi na serikali yao .
Hayo ameyasema jana katika ofsi ya mkuu wa Mkoa – Geita  akiwa katika ziara yake ya siku mbili..........
anayoendelea nayo mkoani Geita  ikiwa na lengo la kuzindua nyumba kumi na nane 18  za waathirika walihamishwa  na mgodi tangu mwaka 2000 kutoka kwenye maeneo yao na kuhamishiwa eneo la Buhalahala walikojengewa na mgodi huo,  ambapo nyumba hizo zenye thamani ya Tsh.  1.2 bilion .
Waziri huyo amesema kuwa baadhi ya maafisa madini nchini wamekuwa na tabia za kutoa lesen za madini ya ujenzi  kwa watu binafsi huku wanaomiliki maeneo hayo vikiwa ni vijiji au vikundi hivyo kuwataka kuacha tabia hizo mara moja.
“Naagiza mimi kama waziri wa Nishati na madini kwa maafisa madini wote Tanzania kutoa leseni za madini ya ujenzi kwa watu binafsi bila kuwashirikisha wanakijiji au vikundi’ , nikisikia afisa madini yeyote anafanya hivyo atafukuzwa kazi mara moja bila kujali cheo chake.  Alisema Simba Chawene
Chawene ameongeza kuwa baadhi ya maafisa madini wanaotoa maeneo ya kuchimba dhahabu kwa wachimbaji wadogowadogo bila kuwa na kitu chochote ndani ya ardhi hiyo nao waache hiyo tabia kwani wanatakiwa kufanya uchunguzi  wa kina kama kuna madini ndo wawapatie hayo maeneo. Endapo kama watabainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Nae mkuu wa mkoa wa Geita Bi.  Fatuma Mwasa akatoa kilio cha wananchi wake mbele ya waziri jinsi mgodi wa Geita Gold Mine unavyowanyima fursa ya tenda katika mgodi huo na badala yake wanatafuta wageni toka nje ili wafanye kazi hizo hali inayosababisha wananchi kuchukia mgodi huo
Mh.  Waziri tunaomba utusadie Geita tunalima mananasi pamoja na mbogamboga lakini tunanyimwa fursa ya kuuza katika mgodi huo na badala yake wanakwenda kuchukua nje na bidhaa zetu zikiozea mashambani.  Alisema Mwasa.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: