.
Ni nyumba ya tatu kutoka kwa mzeee Rweikiza,
.
Waliothirika manispaa bado wanahitaji msaada,
.
Taadhari yaendelea mkoa Kagera.
Familia
nzima ya Bw Jovin Eustace mwenye umri wa miaka 26,mkewe Plasidia Jovin ambaye
alikuwa mjamzito na mwanae Melines Jovin mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu baada
ya kupigwa na radi usiku wa kuamkia leo 16 may 2015, katika kitongoji cha Kiizi
kijiji cha Bulinda takribani kilomita 20 kutoka Bukoba mjini, wakati wa mvua
zilizoanza kunyesha katika maeneo kadhaa ya mkoa wa Kagera usiku huu.
Watu
watatu wa familia moja katika kitongoji kiizi
kijiji cha BULINDA kata kanyangereko halmashauri ya bukoba wameunguzwa
na radi hadi kufa asubuhi ya leo.
Diwani
wa kata hiyo bwana Despikius Mtagahywa akizungumza na mwandishi wa mtandao huu,
amesema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya saa 11:55 alfajiri
Hilo
ni tukio la kwanza kutokea katika kijiji hicho, ambalo limetokea jirani nyumba ya tatu jirani kabisa na
familia ya mzee Samsoni Rweikiza ambaye ni babamzaziwa mbunge wa Bukoba vijiji
Jasson Rweikiza.
Wiki moja iliyopita, mtandao huu uliripoti mafuriko yaliyosababishwa na mvua za msimu huu, ambapo katika manispaa ya Bukoba, familia kadhaa zililazimika kuitaji msaada wa chakula katika kata Miembeni mtaa wa Nyamkazi, ambapo mbunge wa Bukoba mjini kwa ushirikiano wa ofisi ya mkuu wa wilaya, walitoa msaada wa unga kilo 600 na maharage kilo 300.Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment