MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 5 May 2015

JIBU LA NANI ALIOMBA GARI YA ZIMAMOTO BUKOBA: SOMA NA USIKILIZE HAPA

.Ni miongoni mwa zawadi zilizo kwenye mpango Nykobing Mors
.Hakuna ilipotajwa kuombwa na Aman

Mwaka 1983, ndiyo mwaka ambao manispaa ya Bukoba, ilianza urafiki na manispaa ya Nykobing Mors ya nchini Denmark, ambao umekuwa ukifanyika kwa kutembeleana kati ya baadhi ya viongozi wa manispaa hizi mbili, sambamba na kupeana zawadi tofauti kulingana na wakati husika.
Kutokana na urafiki huo, manispaa hiyo imetoa zawadi ya gari ya zimamoto aina ya FALK T703 DDU kwa manispaa ya Bukoba, katika kutekeleza ahadi zake nyingi zilizokwenye mpango wa kuifanyia Bukoba, kama moja na kuonesha ushirikiano uliopo tangu 1983.
2013 ndiyo mwaka ambao uhusiano huo ulifikisha miaka 30 tangu kuanzishwa mwaka 1983, na katika kufanya kumbukumbu ya urafiki huo, Nykombing Mors ilituma mwaliko kwa manispaa ya Bukoba kuwaalika Meya wa manispaa pamoja na madiwani wengine 2 bila kujali meya gani anaongoza ili kuzungumza pamoja kuleta zawadi zilizokuisha aidiwa kwa manispaa ya Bukoba.

Katika kipindi hicho aliyekuwa akiongoza manispaa hiyo tangu 2010 ni Anatory Aman, aliyeongoza ujumbe wa manispaa ya Bukoba kwenye manispaa ya Nykombing Mors nchini Denmark, na kabla ya kuelekea huko, alisoma barua iliyotumwa kwa manispaa ya Bukoba ikiwa ni tarehe 17 may 2013, bonyeza chini kusikiliza alichokwenda kukisema huko na hakuna alipotaja kuwa ataomba gari pamoja na mawazo yaliyotolewa na madiwani, Felician Bigambo, Chief Kalumuna, Mch Mlaki na Mulungi Kichwabuta.
                  

Bw. Samuel N. Luangisa ni nani?
Ni mzaliwa wa Bukoba mmoja kati ya waasisi wa TANU na hatimaye CCM, ambaye alipata kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza wa baada ya uhuru (1961–1964), ambaye hatahivyo alikuwa miongoni mwa waliopendekeza mkoa huo kuitwa Kagera badala ya jina la awali la mkoa wa Ziwa magaharibi.

Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”chini ya ushauriano wa mzee Luangisa.

SAMWEL RUANGISA alipata kuwa mbunge wa jamuhuri ya muungano kupitia jimbo la Bukoba mjini kwa tiketi ya CCM kati ya 1985-1990, na baada ya hapo ameendelea kuwa diwani wa kata Kitendaguro anakozaliwa hadi 2014 alipovuliwa udiwani na mahakama kutokana na mgogoro uliojitokeza na kushindwa kuudhulia baadhi ya vikao vya baraza la madiwani, akiwa miongoni mwa madiwani sita waliovuliwa kati ya madiwani 24 wa manispaa hiyo. 



Manispaa ya Bukoba kwa sasa, inaongozwa na makamu meya mzee Alexander Ngalinda, ambaye anashikilia nafasi hiyo baada ya CAG kutoa taarifa ya uchunguzi wa utekelezaji miradi mbalimbali ya manispaa, na kuonesha kuwa aliyekuwa meya wa manispaa hiyo, kuwa anatakaiwa kujibu baadhi ya tuhuma, na kumtaka kujipima na kujiuzulu, kupitia naibu waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri, aliyesoma taarifa ya waziri mkuu baada ya uchunguzi wa CAG.

Tangu hapo kumekuwa na mvutano katika utoaji wa taarifa za manispaa, kukionesha kazi fulani imefanywa na mtu fulani, ilhali ukweli wa baadhi ya masuala ya msingi ukiwekwa kando.

Na Mwanaharakati.

No comments: