.Kiwango wanachozalisha kwa matajiri kutowiana na mishaara.
.Wasi wasi wa ajira zao baada ya kwenda masomoni na kuachia gari, na
.Kufanya kazi bila mikataba na matajiri/ mashariti magumu ya usalama.
Mtandao huu umefanya mazungumzo
na madereva wa magari ya abiria, kwa lengo la kupata kiini cha mgomo wao,
walipoueleza kuwa wanasubiri hatimaye ya
mambo yao hayo ya msingi.
Ukweli ni kwamba magari haya
yanaingiza kiasi kikubwa kwa matajiri wetu, ambapo kwa safari moja
tunawatengenezea kiasi kikubwa cha pesa, na kutokana na utaratibu tulioelezwa
kuhusu kwenda kusoma, muda wowote unaweza kuachishwa kazi baada ya kuacha gari
kwenda masomoni.
Hatahivyo ukiumia kazini,
unalazimika kujitibu mwenyewe, na kutufanya tufanye kazi kwa mawazo makubwa
kwasababu wakati wowote waweza kupata ajali na usipate msaada wa matibabu.
Mkoa wa Kagera, kuna makampuni
zaidi ya kumi yanayofanya safari za usafirishaji abiria kati ya mikoa ya
Kagera, Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Uganda Nairobi, Kigoma na
kwingineko kote nchini, ambapo baadhi ya madereva waliozungumza nasi kwa
masharti ya kutotajwa majina yao wamesema mgomo huu hasa agenda yake kuu ni
kupata mkataba.
Wamesema kuwa kwa uwiano katika
magari kadhaa kwenda Dra, wanatumia lita kati ya 1200 hadi 1300 za mafuta
ambazo mara nyingi zinampatia tajiri faida y ash milioni 2 kwa tripu moja kama
hakujatokea hitilafu ya gari na inapojitokeza tatizo japo mara moja kwa mwezi
au la anajikuta na faida y ash laki 3, lakini haiwezekani tajiri akapa hasara.
SIKILIZA MALALAMIKO DEREVA
SIKILIZA MALALAMIKO DEREVA
Wakati huo huo wengine wamesema
kuwa barabarani kuna usumbufu mkubwa kwa matrafiki kutokana na tochi,
kuwalazimisha kwenda kwa wakati na baadhi ya askari kulazimisha makosa ambayo
siyo ya kweli ili utoe chochote.
Kwingineko nchini, mgomo huo umetajwa kuendelea mkoa............
Iringa ambapo polisi wamepambana na madereva wa magari na pikipiki baada ya kuonekana boda boda wakibeba abiria ilhali waliogoma hawataki vijana hao waendesha pikipiki kubeba abiria hao.
Katika mji wa Kigoma, habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa baadhi ya madereva wameondoa magari na kubeba abiria, kuashiria kumaliza mgomo wao, japo baadhi ya watu wanasema kuwa wameteseka sana na hali ya mgomo hasa jana.Iringa ambapo polisi wamepambana na madereva wa magari na pikipiki baada ya kuonekana boda boda wakibeba abiria ilhali waliogoma hawataki vijana hao waendesha pikipiki kubeba abiria hao.
Ubungo jijini Dar es salaam, mgomo umeingia siku ya pili, kama inavyoonekana katika picha hii hapa chini.
Mgomo huo ulioanza jana kote nchini, unafanyika huku kukiwa na uitaji wa usafiri kwa abiria waendao mikoani, na kuongza malalamiko kwa jamii ya watanzania huku mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu
SUMATRA, ikisema kuwa wananchi wanasumbuliwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra);- Gilliard Ngewe, alisema, suala hilo lipo katika wizara husika na kwamba kufanyika kwa mgomo huo kutaathiri wananchi kutokana na kukosa huduma za usafiri.
Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, lilimtafuta Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (pichani), bila mafanikio kutokana na simu yake kutopatikana, huku Naibu wake, Charles Tizeba, akisema: “Naomba mnitafute kesho..nipo msibani.”
pia alitafutwa waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka na Naibu wake, Makongoro Mahanga, lakini simu zao hazikuwa hewani.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alikaririwa na vyombo vya habari juzi akisema amepokea ujumbe mfupi wa simu kwamba leo kuna mgomo.
Tishio la mgomo wa leo ni mwendelezo wa mgomo mwingine mkubwa ambao ulidumu kwa takribani saa saba kwa mabasi kutokuruhusiwa kutoka katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi cha Ubungo, Aprili 11, mwaka huu.
Madai ya mgomo huo ambao ulileta adha kubwa kwa wananchi yalikuwa ni kupinga ucheleweshwaji wa malori kwenye mipaka hususani ya Tunduma ambako hukaa kwa zaidi ya siku 26 licha ya kulipiwa kila kitu bandarini.
Mengine ni kupinga sheria namba G 31 ya mwaka 2015 ambayo inazungumzia faini ya Sh. 300,000 au kifungo cha miezi 21 kwa madereva wanapofanya makosa barabarani. Pia kupinga madereva kutakiwa kwenda Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya kujinoa.
Madai mengine yalikuwa ni wamiliki wa magari kutowashirikisha madereva katika mikataba yao ya kazi.
Hata hivyo, mgomo huo ulisitishwa baada ya serikali kupitia kwa Waziri Kabaka kufuta sharti la kwenda chuoni kila baada ya miaka mitatu.
Pia aliahidi kulipatia ufumbuzi suala la mikataba yao katika kikao kilichotarajiwa kufanyika wiki iliyofuata.CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment