Anazungumza na watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari, huku
akieleza kuwa ametangazia Dodoma kwasababu anazungumza na watanzania.
Amesema kuwa matatizo yanayowasibu watanzania hajalisoma vitabuni bali ndiyo maisha aliyoishi, kutokana na umaskini wa alipototea kwenye familia ya mzee Materu, ilhali akisema kuwa alishawahi kubeba zege, na mkewe kupika mama lishe huku akipokea matusi mbalimbali ya wabeba zege wenye njaa.
Mambo matatu muhimu anayofikiri ni muhimu kwaq watanzania, ni kujitegemea hasa kwa kulipa kodi, awamu ya matumizi kwa kuziba mianya ya matumizi mabaya, na kukomesha kazi kwa mazoea.
Ameongeza kuwa tumeendelea kulalamikia masoko, kuuza vitu vikiwa ghafi na kuendelea kulalamikia pembejeo, akisema kuwa kazi ya rais wa tano siyo fadhila bali kazi anayokwenda kuifanya.
Endelea kutufatilia hapa
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment