. Misaada yachelewa
na kutolewa kwa wasiowalengwa,
. Taarifa za maafa
zapotoshwa serikalini,
. Watendaji serikali
watajwa kuvunja taratibu,
. Sheria rasmi yaandaliwa,
baada ya kukiukwa taratibu zilizopo.
Kumekuwa na matukio mbalimbali nchini yanayotajwa kuwa
maafa, jambo linalosababisha lawama kwa mamlaka wahusika wanapokosa msaada,
baada ya kufanyika tathmini na kubainika kuwa siyo maafa kama wanavyokuwa
wakidhaania.
Hatahivyo serikali imejikuta ikipoteza muda na kuwa na
muingiliano na wadau wa kusaidia jamii, huku ikishindwa kug’amua aina ya maafa
kwani kila linapotokea jambo jamii hufikiria kuwa ni maafa, ambapo hayo yote
yanasabishwa na ukosefu wa kitengo cha mawasiliano katika ofisi ya waziri mkuu,
kama anavyofafanua Benedict Kisaka mratibu wa maafa ofisi ya waziri mkuu.
Ukiukwaji wa taratibu za taadhali ni moja ya sababu
zinazoongeza uwepo wa matukio ya majanga na hasa ujenzi holela unatajwa kuwa
sababu kubwa inayosababisha mafuriko katika makaazi ya watu, ambapo imebainika
kuwa wengine wanajenga kwa maelekezo ya maofisa ardhi na mipango miji.
Bi Naima Mrisho ni kaimu mkurugenzi msaidizi idara ya
uratibu wa maafa katika upande wa mipango na utafiti wa ofisi ya waziri mkuu.
Kama kaimu mkurugenzi wa mahafa katika ofisi ya waziri mkuu, nasisitiza hakuna kuendelea kuona watendaji katika taasisi mbalimbali, wanatekeleza kinyume taratibu za nchi, na ndiyo maana tumependekeza kuwa na sheria ya kusimamia maafa ambayo itakwenda sambamba na usimamizi wa kuruhusu watu kujenga katika maeneo yenye utata.Nakiri kwamba wengi wa wanaojenga kwenye vyanzo vya maji, mabondeni na hata kujenga pasipokufuata mfumo wa kitaalamu wanatokana na mamlaka kuwapa maeneo hayo, sasa tutasimamia sheria .
Januari 2014, yalitokea maafa Kilosa mkoani Morgoro ambapo
taarifa iliyosomwa kwa rais na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Joel Nkhaya Bendera
ilikuwa kinyume ikilinganishwa na hali halisi ya maafa, ambapo aliamuru warudie
kufanya tathmini, jambo linalotajwa kuwa ni athari za ukosefu wa kitengo cha
mawasiliano ya maafa wizarani.
Na Mwanaharakati.