MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 30 June 2015

KUSINGIZIA MAAFA KWA UZEMBE WA WATENDAJI TANZANIA, KWAVURUGA WIZARA



. Misaada yachelewa na kutolewa kwa wasiowalengwa,
. Taarifa za maafa zapotoshwa serikalini,
. Watendaji serikali watajwa kuvunja taratibu,
. Sheria rasmi yaandaliwa, baada ya kukiukwa taratibu zilizopo.

Kumekuwa na matukio mbalimbali nchini yanayotajwa kuwa maafa, jambo linalosababisha lawama kwa mamlaka wahusika wanapokosa msaada, baada ya kufanyika tathmini na kubainika kuwa siyo maafa kama wanavyokuwa wakidhaania.
Hatahivyo serikali imejikuta ikipoteza muda na kuwa na muingiliano na wadau wa kusaidia jamii, huku ikishindwa kug’amua aina ya maafa kwani kila linapotokea jambo jamii hufikiria kuwa ni maafa, ambapo hayo yote yanasabishwa na ukosefu wa kitengo cha mawasiliano katika ofisi ya waziri mkuu, kama anavyofafanua Benedict Kisaka mratibu wa maafa ofisi ya waziri mkuu.
Ukiukwaji wa taratibu za taadhali ni moja ya sababu zinazoongeza uwepo wa matukio ya majanga na hasa ujenzi holela unatajwa kuwa sababu kubwa inayosababisha mafuriko katika makaazi ya watu, ambapo imebainika kuwa wengine wanajenga kwa maelekezo ya maofisa ardhi na mipango miji.

Bi Naima Mrisho ni kaimu mkurugenzi msaidizi idara ya uratibu wa maafa katika upande wa mipango na utafiti wa ofisi ya waziri mkuu.
Kama kaimu mkurugenzi wa mahafa katika ofisi ya waziri mkuu, nasisitiza hakuna kuendelea kuona watendaji katika taasisi mbalimbali, wanatekeleza kinyume taratibu za nchi, na ndiyo maana tumependekeza kuwa na sheria ya kusimamia maafa ambayo itakwenda sambamba na usimamizi wa kuruhusu watu kujenga katika maeneo yenye utata.

Nakiri kwamba wengi wa wanaojenga kwenye vyanzo vya maji, mabondeni na hata kujenga pasipokufuata mfumo wa kitaalamu wanatokana na mamlaka kuwapa maeneo hayo, sasa tutasimamia sheria .


Januari 2014, yalitokea maafa Kilosa mkoani Morgoro ambapo taarifa iliyosomwa kwa rais na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Joel Nkhaya Bendera ilikuwa kinyume ikilinganishwa na hali halisi ya maafa, ambapo aliamuru warudie kufanya tathmini, jambo linalotajwa kuwa ni athari za ukosefu wa kitengo cha mawasiliano ya maafa wizarani.

Na Mwanaharakati.

No comments: