MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 30 June 2015

UTATA WA KIFO CHA MWANDISHI EDSONI KAMUKARA KATIKA MAZIKO YAKE MULEBA

. Yatajwa kufariki baada ya kukosa hewa,


Edson Slavatory Kamukara, amezikwa kijijini kwao Ihangiro wilayaniMuleba, huku akiacha majonzi kwa familia yake, baada ya kuacha mtoto mmoja ilhali mama yake akisumbuliwa na kupooza, ambapo siku chache zilizopita, Edson alitokea Muleba kumuangalia mama yake, kama alivyozungumza dada wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Joyce.

Akizungumza katika maziko hayo, mkurugenzi wa kampuni ya mwana halisi publishers LTD Bwana Said Kubenea, amesema kifo cha marehemu Kamukara, kimezua utata kutokana na hakuna anayejua undani,
huku akisema kuwa madakatari wanasema inaonekana alikufa baada ya kukosa hewa huku, chumbani kwake kukikutwa na damu, akiongeza kuwa alikuwa anakamilisha kazi ya uandishi uliokuwa ukiwahusu vigogo na kama habari zake zingetoka, saizi nchi ingekuwa inaongea mambo mengine.




Waadishi kutoka chama cha waandishi  habari mkoani Kagera KPC, walishiriki maziko hayo na ndiyo walihusika kubeba mwili wa marehemu na picha chini ni Charles Mwebeya akitroa rambirambi yao kwao dada Joyce ambaye anaishi Dar na alikuwa karibu na marehemu.
Marehemu Edson Kamukara, ameacha mtoto anakadiriwa kuwa na miaka kati ya 3 hadi 4 aitwaye  Edigar Ishengoma, na marehemu alianzia kazi ya uandishi katika gazeti la Majira, akafanya jambo leo, tanzania dai, na hatimaye mwanahalisi publishers ambapo amefanyia kwa kipindi cha miezi minne, na alikuwa anakamilisha habari kuhusu matatizo ya wananchi kupitia viongozi mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.

No comments: