Imeripotiwa kuwa Raisi wa
Fifa,Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili
kuthibitisha tuhuma za rushwa zinazomkabili katika chama cha ulimwengu
wa soka.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kujiuzulu wadhifa wake.Wakati ambao waendesha mashtaka nchini Marekani wanaoifuatilia kesi hiyo ya uhalifu waliweza kuwakamata maafisa saba wa Fifa nchini Switzerland kati ya watu 14 walioshutumiwa siku mbili baada ya kukamatwa,Bwana Blatter ambaye alikuwa amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa raisi wa Shirikisho hillo la Fifa.
Hata hivyo Blatter,alisema jana kuwa anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani. Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa.
Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema kuwa bado maafisa hao wa marekani wanamatumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa chafu unavyomuhusisha Blatter.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu usimamizi na mizizi ya rushwa katika shirikisho hilo la soka,ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa utafiti na si mwisho.
Huu ni mwanzo wa Fifa pia.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini Marekani na mwanasheria wa wilaya ya Mashariki mwa New York , ambaye alishiriki katika mashitaka hayo walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.
No comments:
Post a Comment