.
Wanadai kulipwa fidia ya nyumba,
.
Mkandarasi aomba siku 45,
.
Ujenzi wa mradi wa maji unaendela,
. Wamuitaji Kagasheki awatetee.

Ni katika kata Bakoba mjini Bukoba, wamesema kuwa Wananchi hao wa kata ya Bakoba wamedanganywa kwa muda mrefu, na hawaelewi mstakabali wa makaazi yao, kutokana na nyumba zao kubomolewa, wakati wakandarasi wakipasua miamba ili kupitisha mabomba ya maji.
Mimi ni mwenyekiti wa mtaa wa Forodhani na nimekuwa nikifuatilia jambo hili kwa kushirikiana na wananchi, hivi leo baada ya wananchi kuona hakuna hatua inayochukuliwa na mkandarasi, wameamua kufunga barabara ili washinikize kufidiwa nyumba zao ambazo hatahivyo hawajaambiwa watafidiwa kiasi gani.
Nimezungumza na mkandarasi akaomba tumbe siku 45, na hii ni CD ya inayoonesha madhara ya nyumba zilizopata nyufa zingfine kubomolewa.

Kwa upande wake muhandis mshauri Fortunatus Kasimbi, amesema hii ni mara yua pili kwa wananchi hao kuandamana, katika kampuni hii kutoka Ujerumani, lakini hayo yanatokana na ulipuaji wa miamba ambayo ilikuwa katika makaazi ya watu lakini tuliwaomba watupe subira, na leo ilikuwa siku ya kukutana nao, lakini wenzetu hawakuanza maafikiano badala yake wamefika na kutufungia barabara.
Tunachowaeleza leo kupitia mkandarasi wangu, watupe siku 45 ili tukamilishe fidia yao, ambayo bado tunaendelea kuifanyia upembuzi tujue nani andai nini.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment