MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 8 July 2015

CHADEMA WAPOTEZA KIONGOZI MANISPAA YA BUKOBA, DOKTA AMANI ASUBIRI MWANASHERIA.



. Aamua kuachana na siasa,
. Asema makundi yapo ndani ya chama,
. Baraza  lavunjwa Aman akisubiri mwanasheria wake.


Ni aliyekuwa diwani wa kata Rwamishenye kupitia CHADEMA, Dismas Rutagwerela, aliyetumikia udiwani kupitia chama hicho kwa miaka 10, ambapo amesema kuwa ameingia kwenye uongozi kipindi mfumo wa vyama vingi ukianza, na sasa umeimarika hivyo naye ameamua kuwa mfano kwa viongozi wengine, ambao wanaanzisha makundi kwa kisingizio cha kuletea wananchi maendeleo.



Bwana Rutagwelela, amesisitiza kuwa ndani ya CHADEMA kumekuwa na mmeguko, ambao hatahivyo haujawa rasmi kwasababu kwenye mikutano wanajinadi kuwa wamoja, lakini baada ya hapo kila mmoja anazungumza jambo lake kitu ambacho hakiwezi kusaidia kuwaletea maendeleo, kama anvyofafanua hapa.


Akizungumzia, kupoteza mwanachama huyo na kiongozi wa kata katika CHADEMA, mwenyekiti wa chama hicho wilaya Bwana Victor Sheljei, amesema kuwa hawezi kumzuia mwanachama kuondoka au kuacha uongozi katika chama kwani ndiyo demokrasia, haijalishi kuna kilicho mkera ndani ya chama au hakipo.








Cahama hicho cha CHADEMA, katika muhula wa 2010-15, kilikuwa na madiwani wane wakiwamo wakuchaguliwa na viti maalumu.
Kuhusu ya Bwana Anatoli Amani ;
Meya ambaye hakumaliza muda wake Anatoli Amani, amlipoojiwa na mtandao huu kuhusu kesi aliyofungua mahakamani ili afunguliwe ofisi, amesema wakili wake ndiyo mwenye majibu kama aendelee na kesi au ndiyo mwisho wake


Akizungumza na mtandao huu, mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Lukiko Chibunu, amesema kuwa fedha zinazotajwa kurudishwa benki ya dunia bilioni 18, zimewekwa kwenye mpango wa mwaka ujao, kwasababu wahisani waliridhia baada ya madiwani kumaliza mgogoro uliokuwapo na kuanza kukaa vikao.
Na Mwanaharakati.

No comments: