MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 4 July 2015

DCI ATUA BUKOBA KWA UCHUNGUZI BAADA YA MTU KUCHINJWA YALIPOANZIA MAUAJI KAGERA


. Ameuawa kata Kagondo,

. Polisi iliahidi kituo imeweka beria ya ushuru,

. Wananchi wahisi kutelekezwa na usalama,

. Waziri asema hili janga la kitaifa.
Waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe, aliyeamuru DCI kufika Kagera jana Julai 03 kuchunguza mauaji hayo.

Miaka miwili iliyopita, ilitokea chinjachinja katika kata Muhutwe wilayani Muleba, ambapo watu sita walipoteza maisha katika vifo vya kufanana, oktoba 9 hadi desemba 11 mwaka 2014, wakauawa watu 7 katika manispaa ya Bukoba kwa vifo vya kufanana, ambapo mwezi machi hadi julai 2015, wane wameuawa katika manispaa ya Bukoba na kusambaa Bukoba vijijini kwa kuuawa watu wawili, na halmashauri ya Misenyi kuuawa watu wawili kwa wakati mmoja.

Mtandao huu ulitembelea kata Muhutwe na Kagondo mwishoni mwa 2012 na kuzungumza na wafiwa na wenyeviti wa mitaa, kama wanavyoeleza kisa kizima hapa
Kuhusu tukio hilo, aliyekuwa kamanda wa polisi mkoani Kagera wakati SACP Philip Kalangi, alikiri kuwapo kwa mauaji ya kutisha na kuahidi kujenga kituo cha polisi chenye idadi ya kutosha ya askari ambao wangefanya doria za mara kwa mara
Mwaka 2013, mganga wa kienyeji alimchinja ,mwanafunzi wa shule ya msingi Fausta Jofrey wa kijiji Bishonde  na kuzika viungo vyake chini ya kitanda chake, ambapo polisi ilifanikiwa kumkamata lakini mauaji hayo yanaonesha kutokoma, kwani usiku wa kuamkia tarehe 1 julai 2015, ameuawa kijana Fabian Kalokora ambapo mwenyekiti wa kijiji Bukoki Joseph John Lweyendera beria iliyowekwa badala ya kituo haijawasaidia chochote tofauti na kukamata mazao
Katika manispaa ya Bukoba, mauaji yalianzia katika kanisa na Pentekoste kata Kitendaguro, ambapo aliuawa mwalimu Dioniz Ng’wandu, wiki moja baadaye akakutwa ameuawa kijana ambaye hakufahamika huku akinyofolewa macho, na baadaye aliuawa Mozes Kashaga kwa kukatwa na kitu cha ncha kali, na kufutia Rutulanisa, Goodruck, na wengine katika kata za Kibeta, Rwamishenye Kagondo na Kashai, na jumla yake kufikia waliouawa 7 katika kipindi cha 06 oktoba hadi 05 desemba 2014.
Baada ya mtandao huu kufanya uchunguzi huo, ilimtafuta kamanda wa polisi wakati huo Henry Mwaibambe, ambaye alikiri uwapo wa mauaji hayo ya kutisha kama anavyoeleza hapaMwendelezo kuhusu vifo vya machi  hadi Julai mwaka huu, utakujia hapa, endelea kufuatilia sehemu ya pili.

Na Mwanaharakati.

No comments: