KUTAJWA TANO BORA
Muda mfupi baada ya kikao hicho, pamoja
na kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
alikataa kutaja majina yaliyopitishwa, akaunti ya Twitter ya CCM, iliwataja
waliopitishwa kuwa ni Bernard Membe, Dk John Magufuli, Dk Asha Rose
Migiro, January Makamba na Amina Salum Ali na kuwatupa
wengine 33 akiwamo Lowassa.
Alipotakiwa kutaja majina ya makada watano waliopitishwa, Nape alisema: “Nimeambiwa mchakato bado unaendelea na kesho (leo) Halmashauri Kuu itakutana kuendelea na kazi. Kwa hiyo nawakaribisha kesho kuanzia saa 4:00 asubuhi mje mchukue picha, habari, karibu sana.” Mkutano Mkuu utafanyika saa nane mchana leo.”
Dakika chache baada ya kikao hicho kumalizika, wajumbe watatu wa Kamati Kuu, wakiongozwa na mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi waliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa wanapinga uamuzi huo ambao hawakuutaja, wakidai kuwa si majina yote yaliyowasilishwa mbele ya kamati hiyo.
Dk Nchimbi, akiongozana na mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sofia Simba waliwaeleza waandishi wa habari mara tu baada ya mkutano wa Kamati Kuu kuwa kikao hicho hakikufuata kanuni kwa kuwa majina machache yaliwasilishwa na hayakuhusisha mgombea anayekubalika.
Ingawa hawakumtaja mgombea huyo waliyesema anatajwa na wengi, wajumbe hao wanafahamika kuwa wanamuunga mkono Lowassa.
SLAHA KUPEPERUSHA BENDERA YA UKAWA;
Hatimaye jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya kamati inayounda kamati kuu ya UKAWA imesema jina la Slaa limepitishwa na idadi kubwa ya wajumbe baada ya kutokea mvutano mkubwa miongoni mwa vyama vinavyounda umoja huo.
Baadhi ya wajumbe wa kamati maalumu inayoongozwa na viongozi wa kitaifa jana walithibitisha kuteuliwa kwa Slaa kwa kueleza kuwa tayari jina lake limeshapitishwa na linatarajiwa kutangazwa rasmi baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo.
Aidha walieleza kuwa watatangaza wagombea wenza.
Ibrahim Lipumba ambaye awali alitangaza kuitaka nafasi hiyo, atautumia mkutano huo baina ya viongozi wa Ukawa kuliondoa jina lake ili kumpisha Slaa kugombea ili kulinda maslahi mapana na mafanikio ya Umoja huo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment