Msemaji wa CCM taifa Nape Nnauye, ameongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita, na kusema kuwa hakuna kikao chochote ambacho kimeshafanyika kuhusu mchakato wa kumpata mgombea urais.
Amesema kuwa mitandao inayorusha taarifa kuwa mtu fulani amepita na mwingine amekatwa siyo sahihi, huku akiongeza kuwa kikao cha kuchuja na kupata tano bora kinaanza saa nne asubuhi leo, na baada ya hapo kikao cha kuwapata tatu bora kitafanyika ili kuwapata leo hii.
Awali kulikuwa na taarifa za kufanyika kikao hicho usku wa kuamkia leo lakini ikashindikana kwa mujibu wa taratibu, lakini pia kubadilika kwa ratiba hii hakutoathiri siku ya mwisho ya kumtangaza mpeperusha bendera ya CCM.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment