MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 20 July 2015

KAGASHEKI AREJESHA FOMU, MAZITO HAYA HAPA

. Ni wanaCCM kutopiga kura za chuki,
. Kuvuja kwa siri za chama,
. Watakatifu walikataliwa hatakuwa yeye?

Balozi Kagasheki alichukua fomu kimyakimya na alitaka kurejesha fomu hiyo kimya lakini ushawishi wa wana CCM Bukoba, wamlazimu kukutana nao ili wahakikishe kuwa kweli amerudisha fomu hiyo.
Wakizungumza baada ya kukusanyika katika uwanja wa Kaitaba wanacha hao waliokadiriwa kufikia 200, wamesema kuwa wameshatoa matamko kwenye kata zao kuwa mzee Kagasheki hana sababu  ya kusimama jukwaani kufanya kampeini za kuomba kura ya maoni kwa wanachama kwani alishajitangaza kwa yale aliyofanya, kilichobaki ni kusubiri wana Bukoba wamlipe kwa shukrani.
Pamoja na kauli zao hizo, Balozi Khamis Sued Juma Kagasheki, amesema kuwa ni wakati wa kuwa wamoja, huku wakiwakataa wanaojaribu kudanganya wananchi kuwa wasiitwe wanyonge, ilhali wanadhulumiwa mali zao huku kauli ya CCM kupitia bendera inaonesha chama hicho ni cha watu maskini.

Watu tisa wamejitokeza kuchukua fomu ya kugombea ubunge ndani ya CCM  manispaa akiwamo Balozi Kagasheki, Mjuni Karaiya, Anatoli Amani, Bi Eriet Projestus,Philibert Katabazi, George Lubaiyuka na Chief Kalumuna ambaye ameshindwa kurejesha fomu hiyo.
Na Mwanaharakati.

No comments: